Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt Philip Mpango akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi ya mwaka 2016
na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017/2018 Bungeni Mjini
Dodoma.
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO DODOMA
JUNI 08/2017
Pato la kila mtanzania kwa mwaka
2016 limeongezeka kwa aslimia 11 kutoka shillingi 1,918,897 kwa mwaka
2015 mpaka kufikia shilling 2,131,299 kwa mwaka 2016.
Takwimu hizi zimebainishwa na
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango wakati akiwasilisha
Bungeni Mjini Dodoma Taarifa ya Hali ya Uchumi ya mwaka 2016 na Mpango
wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017/2018.
Akifafanua kuhusu ongezeko hilo
Mhe. Dkt Philip Mpango amesema kuwa Pato la Taifa kwa mwaka 2016
lilifikia Shillingi million 103,744,606 kwa bei za mwaka husika na kiasi
hiki kiligawanywa kwa idadi ya watu 48,676,698 walipo Tanzania Bara na
kufanya wastani wa Pato la kila mtanzania kufikia kiasi cha Shillingi
2,131,299.
Ameeleza kuwa kwa thamani ya Dola
za Marekani, wastani wa pato la Kila mtu liliongezeka kutoka Dola 967.5
mwaka 2015 hadi Dola 979.1 kwa mwaka 2016 ikionesha kuwa Tanzania
inaelekea kwenye kundi la Uchumi wa kati.
“Serikali inaendelea kutatua
changamoto mbalimbali ili tuweze kufikia Uchumi wa Kati kwa kuongeza
fursa mbalimbali za uzalishaji nchini” alisistiza Mhe. Dkt Mpango.
Mhe. Dkt. Phili Mpango ameongeza
kuwa Serikali imejipanga kuboresha shughuli za uzalishaji wa tija katika
Sekta zinazoajiri hususan katika Sekta ya Kilimo cha mazao,Ufugaji na
Uvuvi.
No comments:
Post a Comment