Friday 30 June 2017

Profesa Makame amekagua ujenzi wa jengo la Tatu la Abiria la uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA

unnamed
Meneja ujenzi wa kampuni ya BAM International, Bw. Rey Blumrick akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wa hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa jengo hilo leo mchana.
1
Meneja ujenzi wa kampuni ya BAM International, Bw. Rey Blumrick akifafanua Jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa  Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo jijini Dar es Salaam.
2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa nne kushoto), akiwa katika pichaa ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), na watendaji mbalimbali mara baaada ya kukagua ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo mchana.
3
Muonekano wa sehemu ya Jengo la 3 la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kukamilika kwake kutawezesha jengo hilo kuhudumia abiria wapatao milioni 8 na nusu kwa mwaka.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua ujenzi wa jengo la Tatu la Abiria la uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na kuelezea kuridhishwa kwake kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo Waziri Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi BAM International anayejenga jengo hilo kuwa Serikali italipa madai yake kwa wakati kwa kadri atakavyoyawasilisha.
“Nia yetu ujenzi huu ukamilike ifikapo Septemba mwakani, hivyo tunamtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi na wasimamizi kumsimamia kikamilifu ili vifaa vinavyofungwa katika jengo hilo viwe na ubora uliokusudiwa na vidumu kwa muda mrefu”, amesisitiza Profesa Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema kukamilika kwa jengo la tatu la abiria la uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kutawezesha uwanja huo kuweza kuhudumia abiria wapatao milioni 8 na  nusu kwa mwaka na hivyo kukuza uchumi wa nchi kwa kuwezesha watalii na wageni wengi zaidi kufika nchini.
 
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Profesa Ninatubu Lema amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi huo unasimamiwa kikamilifu na utamalizika kwa wakati.
“Kama wasimamizi tumejipanga kuhakikisha zoezi la ufungaji vifaa katika jengo hili, linakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa,” amesisitiza Prof. Lema.
Naye Meneja ujenzi wa BAM International, Bw. Rey Blumrick amesema kazi iko katika hatua nzuri na itakamilika kwa wakati.
Mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria ni sehemu ya uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere lengo likiwa ni kuwezesha ndege na abiria wengi kutumia uwanja huu na kuhuisha sekta ya usafiri wa anga hapa nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment