Wednesday 28 June 2017

Qatar yailaumu Saudi Arabia kwa kukataa mazungumzo

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Qatar amewalaumu majirani wake wa Ghuba, kwa kukataa mazungumzo kuhusu matakwa yao, ili kurejesha safari za ndege, baharini na ardhini kwa taifa hilo.
Sheikh Mohammed Al Thani alisema kwa hatua hizo ni kimyume na mahusiano ya kimataifa.
Saudi Arabia, milki ya nchi za kiarabu, Bahrain na Misri, wanaishutumu Qatar kwa kuunga mkono Ugaidi.
Qatar imepewa masharti kadha ambayo waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Saudi Arabia ameyataja kuwa yasiyo jadiliwa.
Hatua ya kuitenga Qatar imezua wasi wa wasi chini Qatar, nchi yenye utajiri wa mafuta na gesi inayotegemea ununuzi wa bidhha kutoka nje kwa watu wake milioni 2.7
Siku ya Ijumaa mataifa hayo manne ya kiarabu yaliipa Qatar orodha ya masharti 13 inayotakiwa iyatimize ili kumaliza mzozo ikiwemo ya kukifunga kituo cha Al Jazeera, kufunga kambi ya jesho la Uturuki, kukata uhusiano na kundi la Muslim Brotherhood na kulegeza uhusiano na Iran.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson, ambaye amejitolea kumaliza mzozo huo amrsema kuwa baadhi ya masharti ni magumu kuyatimiza, lakini kuna mengine ambayo yatahitaji mazungumzo.

Lakini baada ya kufanya mazungunzo na bwana Tillerson mjini Washington, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa saudi, alipokuwa akiulizwa ikiwa matakwa yatajadaliwa alijibu kuwa hayatajadiliwa.

No comments:

Post a Comment