Thursday 22 June 2017

Matumizi ya Nishati Mbadala ya TBL Group Yavutia Wataalamu wa Nishati kutoka Taasisi ya Ujerumani na CTI

unnamed
Meneja wa  kiwanda cha TBL cha ilala,Calvin Martin akiwaelezea wageni mikakati ya kampuni kutumia nishati rafiki wa mazingira
1
Meneja wa  Nishati na Maji wa TBL Group Peter Singisye  (kulia) akifafanua jambo kwa ujumbe wa CTI na    GIZ Sustainable Energy Programme ulipotembea kiwanda cha Ilala .Kutoka kushoto ni  Mshauri  wa matumizi bora ya nishati wa  GIZ Consulting Group,Lydia Koch,Mraribu wa Matumizi ya Nishati  wa  shirikisho la wenye viwanda Tanzania(CTI) Thomas Richard na Msimamizi Mkuu wa matumizi bora ya nishati wa GIZ Sustainable Energy Programme ,Jesper Vauvert.
2
Mtaalamu wa Mazingira wa Tbl Group, Coleta Mamburi (kulia) akifanua jambo kuhusiana na nishati
3
Meneja wa Afya na Usalama  wa TBL Group ,Renatus Nyanda,akielezea  masuala ya usalama kwa wageni hao walipotembelea kiwanda.
4
Wataalamu kutoka TBL Group katika picha ya pamoja na wageni wao baada ya kumalizika ziara

Wataalamu wa masuala ya nishati kutoka Shirika la maendeleo la Ujerumani  (GIZ) na Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda nchini (CTI) wamefanya ziara katika kiwanda cha Tanzania Breweries jijini na kukutana na uongozi na wataalamu mbalimbali wa masuala ya nishati ambapo pia walitembelea sehemu mbalimbali za kiwanda na kujionea  hatua mbalimbali za uzalishaji zinazofanyika kiwandani  hapo.
Ziara hilo ilikuwa na lengo la kujifunza mbinu inazotumia kampuni ya TBL Group kupunguza matumizi ya nishati ya umeme kutoka gridi ya taifa badala yake kubuni uzalishaji mbadala wa nishati ya umeme kutoka vyanzo vingine ambayo tayari imeanza kutumika katika viwanda vilivyopo chini ya kampuni hiyo.
Meneja wa  kiwanda cha TBL cha ilala kilichopo jijini Dar es Salaam,Calvin Martin, aliwaeleza wataalamu hao  kuwa kampuni tayari imeanza kufanya uzalishaji kwa kutumia nishati ya umeme wa jua katika kiwanda cha TBL cha Mbeya na nishati inayotokana na pumba za mpunga katika kiwanda cha TBL Mwanza.
Calvin Martin aliwaeleza wataalamu hao kuwa  matumizi ya nishati hizo mbadala yameanza kuonyesha mafanikio kwa kupunguza gharama za matumizi ya umeme wa kawaida ikiwemo kuwa rafiki wa mazingira.
 
“Kampuni inaendelea na mkakati wa kusambaza matumizi ya nishati hizi mbadala katika viwanda vyake na kutumia vifaa vya uzalishaji vya teknolojia ya kisasa lengo kubwa likiwa ni kupunguza matumizi ya gharama za umeme katika uzalishaji na utunzaji wa mazingira.
Kutokana na ubunifu na jitihada hizi kampuni ya TBL Group mbali na kushinda Tuzo ya  jumla ya Rais ya mzalishaji bora  inayotolewa na Chama cha wenye Viwanda Tanzania (CTI) pia ilishinda katika kipengele cha matumizi mazuri ya nishati (Energy Efficiency Award.

No comments:

Post a Comment