Monday 26 June 2017

Mitandao ya Ohio yadukuliwa na ujumbe wa IS kuchapishwa

Mitandao kadha ya serikali katika jimbo la Ohio nchini Marekani ukiwemo wa Governor John Kasich imedukuliwa na ujumbe wa kuunga mkono kundi la Islamic State kuchapishwa.
Ujumbe huo ulisema , Donald Trump atawajibika kwa kila tone la damu linalomwagika kwenye nchi za kiislamu na kumalizia kusema "Nunaipenda Islamic Stete".


Ujumbe kwenye mtandao ulikuwa na ishara ya kiarabu na ulikuwa maandishi meusi na meupe ambayo hutumiwa kwenyew bendera ya Islamic State.
Ujumbe kwenye mtandao wa Bwana Kasich ulicheza wimbo wa kuitisha maombi ya kiislamu.

No comments:

Post a Comment