Thursday 22 June 2017

Safari ya Mwisho Ally Yanga

  Aliyekuwa shabiki maarufu wa Yanga, Ally Mohammed ‘Ally Yanga’ amezikwa leo nyumbani kwao mkoani Shinyanga baada ya jana kuagwa wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma na kusafirishwa kupelekwa kwao kuzikwa.
Ally maarufu kama Ally Yanga alifariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea Mpwapwa, Dodoma, juzi Jumanne.
Shabiki huyo alikuwa maarufu kwa kujipaka masizi na kuweka kitambi cha bandia pale alipokuwa uwanjani akiishangilia Yanga na wakati mwingine timu za taifa.
Ally ambaye pia alikuwa kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwili wake ulipokelewa na wanachama wa chama hicho kama picha zinavyoonyesha.


No comments:

Post a Comment