Thursday 29 June 2017

Theresa May: Uingereza inahitaji kipindi maalumu kujitoa EU.


Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kwamba Uingereza huenda ikahitaji kipindi maalum cha utekelezaji ili kufanikisha mchakato wa kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya lakini hakutakuwa na kipindi cha mpito kisichokuwa na muda maalum.
May ameliambia Bunge kuwa wakati nchi hiyo itakapofahamu uhusiano wake wa hapo baadaye na Umoja wa Ulaya utakavyokuwa, itahitaji kipindi cha utekelezaji.

Ameongeza kwamba anataka kuweka wazi, kwamba hali hiyo haina maana ya awamu za mpito zisizokuwa na kikomo.
Amesema kwamba Uingereza itajitoa tu na hicho ndicho watu wanachokitaka na ndicho serikali itakachotekeleza.

No comments:

Post a Comment