Wednesday 28 June 2017

Maalimu Seif :Lipumba anataka kufoji nyaraka za Usajili wa Bodi ya wadhamini

Katibu Mkuu wa Chama Cha wananchi CUF amesema kuwa wajumbe wa Bodi ya wadhamini waliosajiliwa na Rita ni feki.
Maalimu Seif amesema kuwa wajumbe hao walipandikizwa na Mwenyekiti anayetambulika na Msajili wa Vyama vya siasa nchini profesa Ibrahim Lipumba.
Maalimu Seif pia ameeleza mbinu zilizosukwa   kumpindua, Mbinu  zilizotumika kutaka kumpindua na kumuondoa ndani ya Chama hicho.
Maalimu Seif amesema kuwa njama hizo ni pamoja na kufoji nyaraka za Usajili wa Bodi ya wadhamini.

Amesema kuwa mipango hiyo imeratibiwa na Msajili wa Vyama vya siasa pamoja na Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambulika na Masajili wa Vyama ambapo mbinu hizo amedai kuzigundua.

No comments:

Post a Comment