Tuesday 20 June 2017

Jose Mourinho awakwaza Mashabiki wa Man U

Ukiwauliza mashabiki wa klabu ya Manchester United ni kitu gani wanakisubiria kwa hamu kubwa hivi sasa baasi ni kumuoma Cristiano Ronaldo anarudi kucheza Old Traford kama mchezaji wao.
Taarifa zinadai baada ya Ronaldo kusema hataki tena kuendelea kucheza nchini Hispania alimuambia wakala wake kwamba angependa kurudi kukipiga katika klabu yake ya zamani ya Manchester United.
Baada ya habari hiyo kulipuka,mashabiki wa United dunia nzima walipatwa na furaha kubwa wakiamini nyota huyo kipenzi chao huenda anarejea nyumbani na kuvaa tena jezi ya Manchester United.
Lakini habari mpya zinadai kocha Jose Mourinho hamtaki Cristiano Ronaldo na badala yake anamtaka Alvaro Morata ndio ajiunge na Manchester United.
Cristiano Ronaldo na Jose Mourinho wakala wao ni mmoja Jorge Mendez na ilitarajiwa itakuwa rahisi kwa Mendez kuwakutanisha pamoja msimu ujao wa ligi kuu ya Uingereza.

Pamoja na Mourinho kutomtaka Ronaldo lakini uhamisho huo unaweza kufanyika kwani familia ya Glazers ambao ndio wamiliki wa timu wanaweza kulazimisha uhamisho huo kutokea.

No comments:

Post a Comment