Tuesday 27 June 2017

Watanzania wapata mualiko wa kuhiji Israel

 Image result for Bodi ya Utalii Tanzania
  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewashauri Watanzania kuchangamkia fursa ya kutembelea maeneo matakatifu nchini Israel kwa gharama nafuu.
Gharama za kutembelea maeneo hayo inayokadiriwa kuwa kati ya Dola za Marekani 1700 na 1800 ambayo ni karibu Sh 3.9 milioni.
Mkurugenzi Mtendaji TTB,  Devota Mdachi amesema wadau wa utalii wa Israel wangependa kuona Watanzania wanatembelea nchi hiyo inayosifika kwa kuwa na maeneo matakatifu.
“Tumetembelea maeneo mengi ya kiroho ikiwemo miji ya Nazareth na Jerusalem, wenyeji wetu wamenipa ujumbe kuwa wanahitaji Watanzania waende wakahiji katika maeneo hayo kwa bei nafuu inayokadiriwa kuwa kati ya Dola za Marekani 1700 na 1800.”
“Fursa hii ni nzuri tafadhali tusiiache kwa sababu mbali ya hija lakini kuna mambo mengi mengine.  Watakaokwenda watakutana na raia wa mataifa mengine watawauliza kuhusu Tanzania, maana yake mtageuka mabalozi wetu na kuvutia watalii wengi zaidi,” amesema Mdachi.


Mdachi amebainisha kiasi hicho cha fedha kinajumuisha nauli ya kwenda na kurudi, malazi pamoja na ziara ya maeneo matakatifu ndani ya miji husika.

No comments:

Post a Comment