Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea msaada wa mablanketi kutoka kwa
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida ukiwa ni msaada kwa ajili ya
waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.Kulia ni Mwakilishi Mkuu
wa Shirika la JICA nchini Toshio Nagase.
Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 6.7m
kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi Taasisi ya wakaguzi wa ndani wa Serikali
na kampuni Binafsi Bw.Richard Magongo leo Jijini Dar es Salaam ukiwa ni
msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea pesa taslimu shilingi milioni 2
kutoka kwa Mwenyekiti wa Magereji Tegeta Bw.Lenard Mwanjela ukiwa ni
msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni
325 kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya ACACIA
ikiwa ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 41.5
kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)
Bw.Ayoub Ryoba ikiwa ni kutokana na harambee iliyofanywa na Shirika la
Utangazaji Tanzania(TBC) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko
la ardhi mkoani Kagera.
Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea moja ya misaada kutoka kwa Katibu
wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa kariakoo Bw.Abdallah Mwinyi ambao
wametoa vifaa vyenye thamani ya milioni 60 ikiwa ni kwa ajili ya
waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amepokea michango yenye thamani ya sh. milioni 660.25 zikiwa ni fedha
taslimu, hundi na vifaa mbalimbali kwa ajili ya wananchi walioathirika
na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, mwezi uliopita.
Makabidhiano ya michango hiyo,
yamefanyika leo mchana (Jumanne, Oktoba 11, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi
ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi hundi ya mfano kwa
Waziri Mkuu, Makamu wa Rais wa kampuni ya ACACIA, Bw. Deodatus Mwanyika
amesema wao wametoa sh. milioni 325 ambazo tayari wameshaziingiza kwenye
akaunti ya maafa.
Amewaomba wadau wengine na
taasisi nyingine hapa nchini wajitokeze kuisaidia Serikali kukabiliana
na janga hili kwani mahitaji halisi ni makubwa kuliko kiasi ambacho
kimekusanywa hadi sasa.
Wadau wengine waliochangia ni
Balozi wa Japan nchini, Bw. Masaharu Yoshinda pamoja na Shirika la
Misaada la Maendeleo la Japan (JICA) ambao wametoa vifaa vyenye thamani
ya sh. milioni 220. Vifaa hivyo ni mahema 220, mablanketi 1,100;
vigodoro vyepesi (sleeping pads) 1,110; madumu ya maji 250 na plastic
sheets 22.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TBC1,
Dk. Ayoub Rioba ambaye alikabidhi hundi za sh. milioni 41.55, amesema
kama taasisi waliguswa na tatizo la maafa ya Kagera kwa hiyo wakatafuta
njia ya kuchangisha ili wapate fedha za kuisaidia Serikali kukabiliana
na tatizo hilo.
“Tuliamua kufanya harambee na
kuwahamasisha wananchi wachangie ambapo wengine walileta kwetu na
wengine wakapeleka moja kwa moja Kagera. Na leo tunakabidhi kiasi
ambacho tulikikusanya kupitia harambee hiyo,” amesema.
Wengine waliokabidhi michango
yao, ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wenye Magereji Tegeta, Bw. Leonard
Mwanjela ambaye ametoa fedha taslimu sh. milioni mbili kwa niaba ya
mafundi gereji wilaya ya Kinondoni. Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Bw. Abdalla Mwinyi amesema walifanya
harambee na kupata sh. milioni 60.8 ambazo wameamua kununua nguo na
magodoro, unga wa mahindi tani 10.
Wengine ni Taasisi ya Wakaguzi wa
Ndani (Internal Audit) ambao wamekabidhi sh. milioni 6.7. Mwenyekiti wa
Bodi wa taasisi hiyo, Bw. Richard Magongo amesema baada ya kuona hilo,
waliamua kuchangishana na kupata kiasi hicho cha fedha.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya
Sura Technologies, Bw. Ramadhar Reddy amekabidhi hundi ya sh. milioni 5
kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokumbwa na maafa hayo.
Akitoa shukrani kwa waliotoa
michango hiyo, Waziri Mkuu amewashukuru wote kwa misaada yao na kuahidi
kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa
walengwa.
“Tunawashukuru sana kwa michango
yote. Kutoa ni moyo na siyo utajiri. Nawaomba Watanzania wengine
muendelee kujitokeza ili tuweze kuwasaidia wenzetu waliokumbwa na maafa
haya,” amesema.
Pia amewashukuru waandishi wa
habari kwa kuwapa wananchi taarifa za matukio hayo na kuwahamasisha
wachangie ndugu zao waliokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi. Tetemeko
hilo lilitokea, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17
na wengine 440 kujeruhiwa.
Pia tetemeko hilo limesababisha
nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi
baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi
126,315 wakihitaji misaada mbalimbali
No comments:
Post a Comment