Shirikisho la Michezo y
a
Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) katika Kalenda ya mwaka 2016
ilipanga michezo ya SHIMIWI ifanyike mkoani Dodoma kuanzia tarehe 14-27
Novemba, 2016.
Kama mnavyofahamu hivi karibuni
Taifa limekumbwa na janga la tetemeko la ardhi Mkoani Kagera. Janga
ambalo limesababisha vifo, limeacha familia nyingi kukosa makazi.
Tetemeko hili limeleta madhara makubwa. Taasisi, Mashirika, nchi
mbalimbali na watu binafsi wameguswa kwa ajili ya kuchangia waathirika
wa tetemeko ili kukabiliana na madhara yaliyotokea.
Katika kutimiza dhamira ya kuleta
maendeleo katika Taifa Serikali ya awamu ya tano imeendelea kuchukua
hatua mbalimbali ili kuleta ufanisi. Zikiwemo kuahirisha Maadhimisho ya
Sherehe za Uhuru ili fedha ambazo zingetumika zielekezwe kwenye miradi
ya maendeleo na vile vile imeelekeza kuhakikisha azma ya kuhamishia
Makao Makuu ya Serikali Dodoma inatimizwa.
Majukumu yote niliyoyataja
yanategemea Mapato ya Serikali. Vile vile gharama za kuendesha Michezo
ya SHIMIWI kwa kiasi kikubwa zinatokana na Bajeti ya Serikali.
Tunapenda kuwaarifu Wananchi, Wanamichezo wote na Watumishi wa Umma wote
kuwa kwa kuzingatia majukumu yote ambayo Taifa inayatekeleza kwa sasa
SHIMIWI imeamua kuunga mkono kwa kuahirisha michezo ya SHIMIWI kwa
mwaka huu 2016 ili kushirikiana kuelekeza nguvu pamoja na makundi
mengine ya kijamii wakiwemo Watumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu
hayo. Tunawashauri watumishi wote waendelee kufanya mazoezi kwa ajili
ya kujenga afya zao kupitia ushiriki wa pamoja kwenye Bonanza la
Wafanyakazi wa Umma katika maeneo yao katika siku za mwisho wa wiki.
Vile vile naomba nitumie fursa hii kusisitiza vilabu wanachama
vihakikishe vinalipa ada ya mwaka kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa mwaka utakaofanyika Januari, 2017. Hadi sasa ni timu chache
zimekwishalipa. Kumbukeni kwamba kwa mujibu wa katiba ya SHIMIWI
wanachama watakaoshiriki kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka ni wale waliolipa
ada ya mwaka.
Daniel Mwalusamba
MWENYEKITI – SHIMIWI – TAIFA
No comments:
Post a Comment