Friday 28 October 2016

Dkt. Ali Mohamed Shein, kesho tarehe 29/10/2016 anatarajia kukiongoza Kikao cha Kamati

shein
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (BLM), Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kesho tarehe  29/10/2016 anatarajia kukiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar – Idara ya Itikadi na Uenezi, Mhe. Waride Bakar Jabu, amesema kikao hicho cha kawaida cha siku moja kitafanyika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Amesema kikao pamoja na mambo mengine, kitapokea na kujadili taarifa mbali mbali kutoka Idara na Vitengo vya Chama hicho na kuongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika.
Aidha, Katibu Waride amesema kikao hicho kilitanguliwa na Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC, kilichokutana tarehe 26 Octoba, mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai, kwa lengo la kuandaa Agenda za kikao hicho.
                               “KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI”
Waride Bakar Jabu
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC
Idara ya Itikadi na Uenezi – CCM
ZANZIBAR.
28/10/2016

No comments:

Post a Comment