Friday 28 October 2016

Rand ya Afrika Kusini yashuka thamani

Waziri wa Fedha wa Afrika kusini Pravin Gordhan
Fedha ya Afrika Kusini Rand imeshuka thamani zaidi kwa siku ya pili, baada ya jana Waziri wa Fedha Pravin Gordhan kupunguza matarajio ya ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo na kubashiri nakisi ya bajeti.
Baada ya kutoa taarifa yake ya bajeti ya kipindi cha kati jana, Randi 13.95 iliuzwa kwa dola moja ikiwa ni kushuka kwa asilimia 0.47 kuliko ilivyokuwa siku ya Jumatano ilipokuwa ikiuzwa kwa Randi 13.89 kwa dola moja.
Hali ya uchumi inatarajiwa kuwa ya hofu zaidi baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo, huku taifa la Afrika Kusini sasa likingojea kusikia kitakachoendelea wakati Waziri Gordhan atakapofika mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili

No comments:

Post a Comment