Wednesday 26 October 2016

Kocha Mkuu Joseph Omog akitamba kuwa wamekuja kuchukua alama tatu muhimu

 Image result for simba timu
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam  tayari imeshatua mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mwadui FC unaotarajiwa kuchezwa mwisho mwa wiki hii huku Kocha Mkuu Joseph Omog akitamba kuwa wamekuja kuchukua alama tatu muhimu.
Akizungumza baada ya kutua Shinyanga Omog,amesema kuwa nia yetu ni kuendelea kupata matokeo mazuri kwa kila mechi tunayokutana nayo na sio kwamba tunadharau wapinzani ila msimu huu tumejiandaa kutwaa ubingwa mapema na hiyo ndio kiu ya wanasimba.
“Tumekuja kupambana na kuondoka na alama zote kwa sababu tuna mechi mbili dhidi ya Mwadui FC na Stand United hivyo hatukuja  kutalii na tunajua michezo yote itakuwa migumu kwetu ila wachezaji wangu wapo kwa ajili ya kupata ushindi”alisema Omog
Kwa sasa Simba ndio timu pekee ambayo imecheza mechi kumi na moja bila kupoteza hata mchezo mmoja na kujikusanyia alama 29 na kuwa kinara wa Ligi huku wachezaji wakiwa na morali na kiu ya kuchukua ubingwa msimu huu na wanaonekana kuwa na uchu wa mafanikio.
Ukiangalia kila idara msimu huu imekamilika na mchezaji yoyote anayeingia anaenda kufanya kazi yake ipasavyo na kumekuwa na wafugaji wengi pindi wanapopata nafasi ya kutupia na kwa sasa wafungaji vinara katika timu hiyo ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin ambaye  ameibuka ghafla na kuwa mwiba mkali kwa magolikipa ambapo  kila mechi anacheka na nyavu tu.

No comments:

Post a Comment