Wednesday 26 October 2016

Kauli ya Kikwete UDSM yazua mjadala

  Mitandao ya kijamii jana ilisheheni sehemu ndogo ya hotuba ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ikieleza mambo ambayo kiongozi mpya anatakiwa kuyafanya.
Kikwete alisema maneno hayo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati akizungumzia mambo anayokusudia kuyafanya akiwa mkuu mpya wa taasisi hiyo.
“Unapokuwa mpya ni lazima watu waone kuna mambo mapya. Lakini mapya ya maendeleo,” alisema na kutulia akiangalia hadhira na baadaye kutabasamu.
“Na sio mapya ya kubomoa kule tulikotoka,” alisema na kutoa kicheko kabla ya kuendelea kusoma hotuba yake iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza.

No comments:

Post a Comment