Monday 24 October 2016

Tanzania imeunda kifaa cha kupimia Mabadiliko ya Hali ya Hewa

Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam – DIT, imebuni mifumo ya TEHAMA na kutengeneza vifaa vya kuchukulia na kupimia Mabadiliko ya Hali ya Hewa  ambavyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji, uchakataji na usambazaji wa taarifa hizo kwa walengwa.
screen-shot-2016-10-24-at-1-08-32-pm
Kubuniwa kwa vifaa na mifumo hiyo kutasaidia kuongeza ufanisi kwa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, ambayo ndiyo mlengwa namba moja wa matumizi ya mifumo na vifaa hivyo vya kurikodi mwenendo wa hali ya hewa.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako, Kesho anatarajiwa kuzindua vifaa na mifumo hiyo itakayoambatana na warsha ya masuala ya Tehama.
Katika soko la Kimataifa, vifaa hivyo vinagharimu zaidi ya Shilingi milion 22 lakini kwa kutengenezwa hapa nchini, vitagharimu zaidi ya shilingi milion nne pekee.

No comments:

Post a Comment