Wednesday 26 October 2016

wakinamama wajawazito mkoa wa Pwani kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya muda mrefu ya kujifungulia wakiwa njiani

mche
Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mbunju na Mbambe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuwatembelea kwa ajili ya  kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

NA VICTOR  MASANGU, RUFIJI
Baadhi ya wakinamama wajawazito wanaoishi katika vijiji vya  Mbunju na Mbambe vilivyopo kata ya Mkongo 
 Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya muda mrefu ya kujifungulia wakiwa  njiani kutokana na kuwepo kwa umbali mrefu kutoka makazi wanayoishi hadi kufika katika zahanati au  kituo cha afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wakinamama hao wametoa kilio chao wakati walipotembelewa na mbunge wa jimbo la Rufiji ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi yenye  lengo la kuweza kusikiliza changamoto  mbali mbali zinazowakabili wananchi wake  pamoja na  kero zao  ili  kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mikakati ya kuleta chachu ya maendeleo.
Zarau Kiambwe  Tabia Athumani,pamoja na Suzan Masela  ni miongoni mwa wakinamama hao wanaokabiliwa na changamoto hiyo,walisema  wakati mwingine wanapata wakati mgumu hususan nyakati za usiku kutokana na kukosa usafiri hivyo kuwalazimu kujifungulia njiani hali ambayo inahatarisha uhai wa kupopteza maisha yao ukizingatia na gharama za usafiri wa piki piki ni kubwa hivyo wanashindwa kuzimudu kutoka na kutokuwa na kipato chochote.
Aidha wakinamama hao wamemuomba Mbunge wa jimbo hilo la Rufiji kwa kushirikianana serikali ya awamu ya tano kuliingilia kati suala hilo ili kuweza kuwasaidia wananchi kwa  kuwajengeaa  zahanati pamoja na vituo vya afya vilivyvyo karibu na maeneo wanayoishi ili kuweza kupata huduma ya matibatu kwa urahisi bila ya  usumbufu.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa baada ya kusikiliza kilio cha siku nyingi kutoka kwa wakinamama hao amesema kwamba  atahakikisha anashirikina bega kwa bga na viongozi wa halmashari pamoja na serikali katika kujenga zahanati na vituo vya afya sambamba na kuongeza idadi ya wauguzi pamoja na madaktari.
Mchengrwa alisema kwamba  katika kuunga juhudi za  serikali katika kuboresha sekta ya afya atahakikisha anaweka mipango madhubuti kwa kuongeza idadi ya ujenzi wa majengo ya huduma za afya ili kuweza kuwafikia kwa urahisi wananchi katika upatikanaji wa  matibabu bila ya kusafiri kutembea umbali mrefu.
“Dhamira kubwa ya serikali hii ya awamu ya tano ni kuhakikihs huduma ya afya inakuwa karibu na jamii ambayo inatuzunguka, hivyo kwa upande wangu kama Mbunge wa Jimbo hili la Rufiji nitakuwa mstari wa mbele katika kushirikina na viongozi wa halmashauri lengo ikiwa ni kuwaondolea kero wananchi ya kufuata huduma mbali, hivyo katika hili nitalisimamia kwa hali na mali,”alima Mchengerwa.
Changamoto ya baadhi ya wakinamama katika maeneo mbali mbali ya Wilani Rufiji Mkoani Pwani ya kujifungulia wakiwa njiani bado inaonekana bado kuwa ni tatizo sugu na hii  ni kutokana na kuwepo kwa umbari mrefu wa kuzikia  zahanati pamoja na vituo vya afya hivyo kusababisha kero na usumbufu mkubwa pindi mgonjwa anapohitajika kupelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu hivyo ni jukumu la serikali kuboresha sekta ya afya katika kukabiliana  na hali hiyo.

No comments:

Post a Comment