Saturday 29 October 2016

Mjumbe wa Shirikisho la Soka Afrika,Said El Maamry kumaliza mgogoro wa beki Hassan Ramadhani Kessy

said-el-maamry
Mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Soka Afrika,Said El Maamry

Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Soka Afrika,Said El Maamry anatarajia kuwakutanisha viongozi wa Simba na Yanga ili kumaliza utata wa beki Hassan Ramadhani Kessy na kuotoa mgogoro uliopo katika usajili kwa pande zote mbili.
El Maamry anakutana na pande hizo mbili kujadili suala la beki Hassan Kessy ambaye Simba inamlalamikia kusajili na Yanga huku akijua ana mkataba na wana msimbazi na Kessy anailalamikiwa Simba.
“Kweli El Maamry amekubali na leo, ndiyo tunakutana kwa ajili ya kulimaliza suala hilo na Simba,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga kutoka makao makuu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam.
  Alisema kuwa Lengo letu ni kulimaliza hili suala, kwa kuwa hii nafasi ya El Maamry ni nzuri kwa maana hiyo ya kulimaliza, tunaamini tutafikia mwafaka na kumuacha mchezaji akili yake awaze mpira tu na sio mambo mengine.
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ambayo inashughulikia suala hilo, ilitoa nafasi kwa Yanga na Simba kufikia mwafaka kabla yenyewe haijatoa maamuzi.
Lakini kama Yanga itashindwa na kuamliwa kulipa, itakuwa tatizo kwao kwa kuwa tayari imeshamtumia Kessy katika mechi kadhaa za ligi kwa upande mwingine msemaji wa TFF alishawahi kusema kuwa ishu ya Kessy sio usajili na kuwaondoa mashabiki wa Yanga kuwa hawawezi kukatwa pointi zozote kwani usajili wake ulipitishwa. Beki huyu ameingia matatani na klabu yake ya zamani yaani Simba kwa madai kuwa alivunja mkataba na kujiunga na Yanga huku akijua kabisa ni kosa hivyo kamati itatoa uamuzi sahihi na sio wa kukomoana hekima na busara zitatumika kumaliza suala hilo ambalo limekuwa ngumzo kwa wadau.
Baada ya kamati hiyo kukaa na kupata maamuzi, iliona inawezekana pia Yanga na Simba kukutana na kulimaliza suala hilo badala ya kutoa maamuzi ambayo yatakuwa yanauumiza upande mmoja

No comments:

Post a Comment