Baadhi ya madereva pikipiki
Chalinze ,wajitokeza kwenye maandamano kuungana na kikosi cha usalama
barabarani mkoani Pwani,kwenye uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama
barabarani,yaliyofanyika viwanja vya polisi Chalinze(Picha na Mwamvua
Mwinyi)
Kamanda wa polisi mkoani
Pwani,Boniventure Mushongi,akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya nenda
kwa usalama barabarani,mkoani humo,yaliyofanyika viwanja vya polisi
Chalinze(Picha na Mwamvua Mwinyi).
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Kamanda wa polisi mkoani Pwani
,Boniventure Mushongi,ameiasa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi
ikiwemo kufunga barabara ama kupiga vibiriti magari kwani kwa kufanya
hivyo ni uvunjifu wa amani.
Aidha amewataka madereva pikipiki(bodaboda)kuacha mbwembwe wawapo barabarani na kutumia vilevi ili kuepukana na ajali zembe.
Aliyasema hayo katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoani Pwani,yaliyofanyika viwanja vya polisi Chalinze.
Kamanda Mushongi alisema kwasasa
wataendelea kuwa wakali kudhibiti vitendo mbalimbali vinavyoashiria
uvunjifu wa amani na kudhibiti ajali hususan barabara kuu.
Alisema ifikie wakati sasa watu kufuata sheria badala ya kupelekea madhara kwa wengine wasio na hatia.
Alieleza kuwa hivi karibuni
kuliwahi kutokea matukio yaliyohusisha wananchi kufunga barabara kwa
masaa kadhaa,ikiwemo WAMI wakidai polisi haina ushirikianao nao hali
iliyosababisha kero kwa madereva na wasafiri waendao mikoani.
Kamanda Mushongi alisema endapo kuna mtu ataona hatendewi haki achukue hatua za kisheria na sio kubughudhi watu wengine.
“Askari mmoja anahudumia watu
1,500 unategemea wakati wewe umekutwa na tatizo muda huo kuna wengine
wangapi wanakuwa na tatizo kama wewe”
“Ifikie hatua ya kuoneana huruma
na kujali kazi za mwingine kwani ukiambiwa atashughulikia suala lako ni
kwamba inahitaji muda ili kila mmoja apate huduma stahiki”alisema
kamanda Mushongi.
Alieleza kwamba jeshi la polisi
lipo pamoja na watu ili kuhakikisha wanalinda usalama wa raia na mali
zao na kuwasaidia pale panapohitajika .
Akizungumzia suala la madereva
bodaboda kupata ajali alisema serikali iliruhusu pikipiki kutumika kama
chombo cha usafiri rahisi nchini na kuwatengenezea ajira vijana wasio
na ajira.
Kamanda mushongi alisema lakini
waendesha pikipiki wengi wamevamia biashara hiyo bila kuwa na mafunzo ya
kuendesha hivyo imekuwa janga la taifa kwa kupata ajali nyingi za vifo
na majeruhi.
“Tunapoteza nguvu kazi kubwa kwa
vijana hawa kufanya mzaha wawapo barabarani wengi wao wamevamia tuu
fani hii,hawana mafunzo ya udereva.
Kamanda huyo aliiomba kamati ya
usalama barabarani mkoani humo kutoa elimu za kutosha kwa jamii kuacha
kujichukulia sheria mkononi kwa kuchoma magari na kufunga njia ovyo.
Hata hivyo aliitaka kamati hiyo kuendelea kutoa mafunzo kwa madereva bodaboda ili kuondokana na ajali za mara kwa mara.
Nae katibu wa usalama barabarani
mkoani hapo,Abdi Issango ambae pia ni kamanda wa usalama barabarani
mkoa,alieleza kuwa watu 165 wamekufa kutokana na ajali za barabarani
zilizotokea katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2016.
Isango alisema vifo hivyo ni pungufu ya watu 18 ikilinganishwa na vifo vya ajali katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2015.
Isango alisema vifo hivyo ni pungufu ya watu 18 ikilinganishwa na vifo vya ajali katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2015.
“Vifo hivyo vimetokana na ajali
376 ambazo ni pungufu kwa asilimia 6 huku watu 402 walijeruhiwa na kuwa
na upungufu ya watu 235 na vifo vilikuwa 148 ongezeko ikiwa ni 10
katika kipindi cha mwaka 2015,”
“Madereva waliokufa walikuwa 27 ikiwa ni ongezeko la madereva 14 ikilinganishwa na waliokufa kipindi kama hicho walikuwa 13 ongezeko likiwa ni asilimia 107.6 ,abiria waliokufa walikuwa 36 pungufu ikiwa ni vifo 39 sawa na asilimia 52 wapanda baiskeli vifo vilikuwa 13 ongezeko la vifo 11,” alisema Issango.
katika kipindi cha mwaka 2015,”
“Madereva waliokufa walikuwa 27 ikiwa ni ongezeko la madereva 14 ikilinganishwa na waliokufa kipindi kama hicho walikuwa 13 ongezeko likiwa ni asilimia 107.6 ,abiria waliokufa walikuwa 36 pungufu ikiwa ni vifo 39 sawa na asilimia 52 wapanda baiskeli vifo vilikuwa 13 ongezeko la vifo 11,” alisema Issango.
Issango alisema Pwani ni moja ya
mikoa yenye ajali nyingi za barabarani hapa nchini kutokana na Jiografia
kwani magari yote yatokayo Dar es Salaam kwenda mikoani na nchi jirani
kwenda Jijini Dar es Salaam
Akielezea changamoto ya barabara
kuu ya Dar es salaam-Chalinze aliiomba serikali kuipanua barabara hiyo
ambayo ni finyu kwani wakati mwingine barabara ufunga na kusababisha
foleni na ajali.
Alitaja tatizo jingine ni ukosefu
wa breakdown ya serikali hasa barabara ya Dar es salaam /Chalinze hivyo
kunapotokea ajali basi trafiki hupata shida kuyatoa.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo
Injinia Michael Mrema ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia
Evarist Ndikilo alisema suala la ukosefu wa breakdown na ufinyu wa
barabara atalifikisha kwa mkuu wa mkoa kwa hatua zaidi.
Alisema awali kulikuwa na tatizo
la mabonde na barabara kuwa mbaya eneo la mlandizi hadi Chalinze lakini
wakala wa barabara TANROADS imelitatua tatizo hilo.
Mrema alisema kwasasa serikali
inaendelea na mipango mingine ya kuboresha na kujenga barabara na
kupanua ikiwemo barabara hiyo ambayo inatarajiwa kuwa barabara ya njia
sita miaka ijayo.
Alikipongeza kikosi cha usalama
barabarani kwa kuendelea kukabiliana na makosa ya usalama barabarani kwa
lengo la kupunguza ajali ambapo alikitaka kuendelee kufanya kazi kwa
juhudi ili kuondoa tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment