Thursday 27 October 2016

Wakati Simba ikiitolea macho Mwadui, Stand United wanaisubiri kwa hamu waitoe shoo

Kocha wa Stand United, Athumani Bilal amesema wanajua ugumu wa mechi dhidi ya Simba, lakini wanachotaka ni pointi tatu.Tokeo la picha la Stand United
Simba itacheza na Stand United Novemba 6 ikiwa ni siku chache baada ya kucheza na Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Stand United ndiye timu pekee ambayo imeshinda dhidi ya vigogo ambao ni Yanga na Azam FC na wote imewafunga kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Bilo ambaye ni beki wa zamani wa Shinyanga Shooting amesema wanajua Simba wana timu mzuri lakini wao wana kikosi bora na wata[ata nafasi zaidi ya kuiona ikicheza na Mwadui.
“Lazima iwe mechi ngumu, hata sisi tunalijua hilo. Lakini kikubwa kwetu tukiwa hapa nyumbani tunachotaka ni pointi tatu,” alisema.

No comments:

Post a Comment