Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao kilichokutanisha
wawakilishi kutoka kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB), Ubalozi wa Sweden na Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na
Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe.
Wawakilishi kutoka Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB), Ubalozi wa Sweden na Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa (UNDP), wakifuatilia maelezo yaliyokuwa
yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
(hayupo pichani) katika kikao hicho.
Wawakilishi kutoka Wizara ya
Nishati na Madini na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC)
wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi Mkazi wa na
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (hayupo
pichani) katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mkazi wa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akisaini kitabu cha
wageni katika Ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo ( wa nne kutoka kulia) katika picha ya pamoja
na wawakilishi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Ubalozi wa
Sweden na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
No comments:
Post a Comment