Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema Shirika la Taifa Maendeleo ya Viwanda (NDC) ndio injini ya kushikiria sekta ya viwanda na hivyo inatakiwa kuhakikisha ndani ya miaka minne inakuwa viwanda hata vitatu katika kuweza kufikia uchumi wa kati.
Mwijage ameyasema hayo leo wakati
wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi NDC, amesema kuwa bodi lazima
ifanye kazi kuhakikisha inashikiria viwanda vikubwa ambayo vitafanya
taifa kuwa na maendeleo ya kiuchumi kutokana miradi iliyopo chini ya
NDC.
Amesema kuwa mradi wa kwanza ni
ule wa Liganga na Mchuchuma unatakiwa kufutika midomoni mwa watu kwa
kuanza kuzalisha kutokana na muda mrefu umekuwa ukizungumzwa.
Mwijage amesema kuwa kutokana
bodi hiyo kuwa na watu wa kila sekta muhimu hivyo wanahitaji kukutana
mara kwa mara hata bila kulipwa posho ili mambo yeande na kuleta tija
kwa taifa.
Amesema kuwa miradi mikubwa
ikikamilika nchi itakuwa imepiga hatua kimaendeleo na kuweza kufikia
uchumi wa kati wa viwanda vyenye kwa wananchi.
Nae Mwenyekiti wa bodi wa NDC,
Dk, Samwel Nyantahe amesema kuwa watafanya kazi kwa karibu na wizara
ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi yote na kuweza kuanza kufanya kazi
kwa nguvu.
Amesema Rais Dk. John Magufuli amemuamini hivyo watatimiza wajibu kwa kushirikiana na bodi hiyo katika sekta ya viwanda.
No comments:
Post a Comment