Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mhandisi John Kijazi, akipeana mkono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango, Bw. Doto James, wakati wa tukio la kuapishwa kwake Ikulu,
Jijini Dar es salaam, Septemba mosi 2016
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James, akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es
salaam, Septemba mosi 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, akitia saini kiapo cha Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, mara baada ya kuapa,
Ikulu, Jijini Dar es salaam, Septemba mosi, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kulia), akiwa katika picha ya
pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, mara
baada ya tukio la kuapishwa kwa Katibu Mkuu huyo, Ikulu Jijini Dar es
slaam, Septemba Mosi, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati), akiwa katika picha
ya pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto kwake), Katibu
Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi (wa nne kushoto), Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto kwake), Naibu
Katibu Mku wizara ya Fedha na Mipango Doroth Mwanyika (wa tatu kushoto),
Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata (wa nne kutoka kulia) pamoja na
maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na mipango, mara baada ya
kuapishwa kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ikulu, Jijini Dare salaam,
Septemba Mosi, 2016
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha
na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Bw. Doto James, mara baada ya kuapishwa na Mhe. Rais
Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu, Jijini Dar es salaam, Septemba mosi,
2016
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James, akila kiapo cha uadilifu mbele ya Kamishna wa
Maadili Jaji (Mst) Salome Kaganda, mara baada ya kuapishwa kushika
wadhifa huo na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es
salaam, Septemba mosi, 2016.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James, akipeana mkono na Kamishna wa Maadili Jaji
(Mst) Salome Kaganda, mara baada ya kula kiapo cha uadilifu baada ya
kuapishwa kushika wadhifa huo na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli,
Ikulu Jijini Dar es salaam, Septemba mosi, 2016.
Katibu wa Chama cha wafanyakazi
TUGHE, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenjeri James, akimkabidhi Katibu
Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, mara baada ya
kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam,
baada ya kuapishwa Ikulu ya Magogoni, kushika wadhifa huo.
(Picha Zote na Wizara ya Fedha na Mipango)
…….
Benny Mwaipaja, MoFP Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemwapisha Katibu Mkuu mpya wa
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, Ikulu, Jijini Dar es
salaam, baada ya kumteua kushika wadhifa huo jana.
Baada ya kuapishwa, Katibu Mkuu
huyo amekula kiapo kingine cha maadili mbele ya Kamishna wa Maadili,
Jaji (Mst.) Salome Kaganda, ambaye amemtaka kutekeleza majukumu yake kwa
uadilifu mkubwa ili kuisaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwatumia
wananchi katika sekta ya fedha na uchumi
Bw. Doto James anachukua nafasi ya
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Servacius Likwelile, ambaye
Mhe. Rais Dkt. Magufuli, amesema atampangia kazi nyingine.
Doto James, ambaye kitaaluma ni
mchumi, alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango
akishughulikia sera, atawaongoza manaibu makatibu wakuu wengine watatu
walioko katika Wizara ya Fedha na mipango.
Tukio hilo limehudhuriwa pia na
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi
John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Peter Ilomo, Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, na wakuu wa Mamlaka na
Taasisi mbalimbali za serikali.
No comments:
Post a Comment