Stella Pius Afisa Mawasiliano wa
Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel akizungumza na waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo kuhusu kampeni ya Madawati
mkoani Tabora , katikati ni Mwenyekiti wa Dr. Amon Foundation Bw. Amon
Mkoga na kushoto ni Ngo Duy Truong Meneja Masoko Halotel
Mwenyekiti wa Dr. Amon Foundation
Bw. Amon Mkoga katikati , Ngo Duy Truong Meneja Masoko Halotel,
Kushoto na Stella Pius Meneja Mawasiliano wa Halotel wakionyesha kwa
waandishi wa habari Bango maalum linaloelezea kampeni ya Simama Kaa
Desk itakayofanyika mkoani Tabora na Pwani.
NA HERIETH HASSAN
Mwenyekiti wa Dr. Amon Foundation
Bw. Amon Mkoga ametoa mchango wa madawati katika kampeni ya
uchangiaji madawati kwa udhamini wa mtandao wa simu za mkononi wa
Halotel hii leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini
Dar-es-Salaam.
Akizungumza na waandishi wa
habari Amon Mkoga amesema kuwa ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ,wameandaa kampeni ya
“Simama Kaa Desk” Kampeni., itakayosaidia kupunguza uhaba wa madawati
ikidhaminiwa na Kampuni ya Simu ya Halotel.
“Lengo kubwa la kampeni hii ya
“Simma Kaa Desk” ni kuchangia na kupunguza upungufu wa madawati
katika shule za msingi na sekondari ili kumuunga mkono rais wa
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Kampeni hiyo itaanzia katika mkoa wa
Tabora na Pwani tukiwa pamoja na Kampuni ya Halotel.”
Aidha afisa mawasiliano wa
Halotel Stella Pius amesema kuwa Halotel itakuwa pamoja na Dr Mkoga
Foundation kuhakikisha kwamba watakuwa bega kwa bega ili kuwasilisha
mchango wa madawati katika elimu.
“Ikiwa ni pamoja na kuunga mkono
uchangiaji wa madawati Haloteli tutahakikisha katika kampeni hii ya
Simama Kaa Desk kampeni, tunawakilisha mchango wetu tukishirikiana na
Dr Amoni Foundation kupitia kampeni hii ambapo tunaamini kuwa ni njia
pekee ya kupunguza uhaba wa madawati mashuleni.”
Licha ya hayo pia kutakuwa na
burudani ya mziki wakati wa kukabidhi madawati hayo ambayo italetwa na
kundi la muziki wa kizazi kipya la Mabaga Fresh la jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment