Mwenyekiti wa Kampuni ya Skol
Building Contractors Limited Bw.Vincent Massawe (kushoto) akikabidhi
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye(kulia)
kiasi cha Shilingi Milioni Kumi taslimu leo jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kusaidia wakazi wa Mkoa wa Kagera waliyoathirika na tetemeko la
ardhi liliotokea hivi karibuni.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akifurahia jambo mara baada ya
kupokea msaada wa Shilingi Milioni Kumi uliyotolewa na Kampuni ya SKOL
Bulding Contractors Limited Ofini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili
ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera
hivi Karibuni (Kushoto) ni Bw.Vincent Massawe kutoka Kampuni hiyo mara
baada ya kukabidhi pesa hizo.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Skol
Bulding Contractors Limited Bw.Vincent Massawe akitoa wito kwa wadau
mbalimbali wa sekta binafsi kujitokeza kutoa msaada wa kuisaidia kwa
ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera alipofika ofisini
kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye
(hayupo pichani) kumkabidhi kiasi cha Shilingi Milioni Kumi leo jijini
Dar es Salaam.
Na Shamimu Nyaki – WHUSM -Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea kiasi cha Shilingi Milioni
Kumi kutoka Kampuni ya Skol Building Contractors Limited.
Akipokea fedha hizo leo Jijini
Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw. Vincent Peter
Masawe Waziri Nnauye amemthibitishia kuwa pesa hizo zitawasilishwa
kwa waathirika wa tetemeko hilo ili zitatue changamoto zinazowakabili.
“Ninashukuru sana kwa msaada wenu
mmetambua changamoto wanazopata wenzetu,niwaombe Watanzania wote
tuendelee kujitoa kuwasaidia ndugu zetu waliopata maafa haya”.Alisema
Mhe.Nnauye.
Aidha Mwenyekiti wa kampuni hiyo
Bw.Vincent Peter Masawe amesema Kampuni yao imeguswa na matatizo
waliyopata wakazi hao wa Kagera na ndio maana wameamua kuwasaidia ili
hali zao za maisha zireje kama zamani.
“Tumeamua kuwasaidia wenzetu na
tunaomba wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla popote walipo waguswe
na jambo hili na waunge mkono Serikali katika juhudi zake za kuwasaidia
waathirika wa tetemeko hili”. Aliongeza Bw.Masawe.
Katika hatua nyingine Mhe. Waziri
amewakaribisha wananchi wote katika harambee ya kuchangia waathirika
hao iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) itakayofanyika
Septemba 21 mwaka huu jioni katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo
Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment