Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mh. Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na Baadhi ya Wabunge wakati
wakiingia wakiingia katika ukumbi wa bunge kuhudhuria kikao cha 2 cha
bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiingia bungeni leo saubuhi.
Mbunge wa Jimbo la Urambo
Mhe.Margaret Sitta akimueleza Jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Mjini Dodoma.
aibu Waziri Wizara ya Fedha na
Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali wakati wa kikao cha 2 cha bunge
la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alitoa wito kwa waajiri
nchini kuwasilisha nyaraka za wastaafu kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii
miezi mitatu hadi sita kabla ya kustaafu kwa wateja wao ili kukabiliana
na changamoto zinazoweza kujitokeza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba Leo Bungeni
Mjini Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kintinku mkoni Singida wakifuatili vikao vya Bunge leo Mjini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijibu swali wakati wa
kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alisema
serikali haina mgogoro wowote wa mafuta baina ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Mjini
Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Kazi, Ajira, Wazee na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (MB)
akimueleza jambo Mwansheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju leo
Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mhe.
Magdalena Sakaya akiuliza swali wakati wa Kikao cha Pili cha Bunge la 11
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
PICHA NA HASSAN SILAYO
No comments:
Post a Comment