Bw Richard Kayombo Mkurugenzi wa
Huduma na Elimu ya Mlipakodi TRA akizungumza na waandishiwa habari
katika makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es salaam leo kuhusu
mikakati hiyo.
Bw Richard Kayombo Mkurugenzi wa
Huduma na Elimu ya Mlipakodi TRA akisisitiza jambo katika mkutano huo
wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Katika harakati za kuhakikisha
kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati, Mamlaka ya
Mapato Tanzania TRA imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuongeza wigo wa
vyanzo vya Mapato pamoja na kukusanya Mapato kikamilifu.
Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo;
Kulifanya eneo la Kariakoo kuwa
Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha biashara
hapa nchini na kuhakikisha kila mfanyabiashara anakuwa na Mashine ya
Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.
Katika kutekeleza hilo Mawakala
wote wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja katika jengo la Al-Falah Towers
lililopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo ili kurahisisha upatikanaji wa
mashine hizo na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika
matumizi ya mashine hizo.
Aidha Mkurugenzi wa Huduma na
Elimu kwa Mlipa kodi TRA Bw. Richard Kayombo ametoa wito kwa wananachi
na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa zao za usajili wa TIN
kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo vifuatavyo kwaajili ya
zoezi hilo kwani muda hautaongezwa baada ya tarehe hiyo maana baada ya
tarehe hiyo zoezi hili litahamia mikoa mingine;
Vituo hivyo vya uhakiki ni pamoja na:
- Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
- Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara
- Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu
- Wilaya ya Kigamboni – Ofisi za TRA Kigamboni
Pamoja na kuhakiki taarifa zao,
wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini wanaombwa kufika katika
ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili kuepuka kukumbwa na msako
unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na uhamasishaji
Wakati huo huo Bw. Kayombo
amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kutekeleza agizo la Serikali
la kufunga mashine za EFDs kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2016
kwani kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe 1 oktoba
na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka
agizo hilo.
Katika kuhakikisha kwamba kodi ya
ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa Wakati Mamlaka inawakumbusha
walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani -VAT
kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla au tarehe 20 ya kila mwezi badala
ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka hu wa fedha.
Kwa upande wa walipa kodi zaa
makadirio na kodi za makampuni (Corpoaration Tax) wanakumbushwa kulipa
kodi zao mapema mwezi hu wa tisa badala ya kusubiri msongamano mwisho wa
mwezi ambao unaweza kuwasababishia usumbufu
Hivyo hivyo walipakodi wote
wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo wanakumbushwa
kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli za TRA
zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.
Kutokana na mikakti mizuri
iliyowekwa na uiongozi wa TRA na serikali Mpaka sasa baadhi ya mikakati
hiyo imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo ambapo
kwa kipindi cha mwezi Agosti 2016 TRA imekusanya Trillioni 1.158
ikilinganishwa na lengo la Trillion 1.152 ambayo ni asilimia 100.57.
ambapo Mwezi Agosti Mwaka 2015 TRA ilikusanya Billion 923.
Wito wetu kwa wanahabari na
wananchi kwa ujumla ni kuendelea kutuunga mkono kwa kuhimiza kutoa
risiti pamoja na kudai risiti katika kila manunuzi pamoja na kutoa
taarifa za dalili za ukwepaji wa kodi wa aina yoyote mahali popote
nchini
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
Richard Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
No comments:
Post a Comment