
Jaribio hilo la Ijumaa lilikuwa kubwa zaidi kuwahi kufanywa na Korea Kaskazini.
Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema bado kuna shimo la kulipua bomu ambalo halijatumiwa katika eneo la kufanyia majaribio Punggye-ri ambalo linaweza kutumiwa kulipua bomu la sita wakati wowote.
Korea Kaskazini ilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa baada ya jaribio hilo la Ijumaa na hali ya wasiwasi na uhasama imeongezeka.
Jumapili, mmoja wa maafisa wa jeshi la Korea Kusini alinukuliwa na shirika la habari la taifa hilo Yonhap akisema kwamba nchi hiyo ina mpango wa kuuangamiza kabisa Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini, iwapo kutaonekana dalili kwamba nchi hiyo inajiandaa kutekeleza shambulio la kinyuklia.

Jumatatu, shirika la Yonhap lilimnukuu afisa mmoja wa serikali akisema dalili zinaonesha Korea Kaskazini imekamilisha maandalizi ya kutekeleza shambulio jingine milimani kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment