Tuesday, 13 September 2016

Clinton afunguka kuhusu ugonjwa wake

Siku moja baada ya mgombea wa urais, nchini Marekani Hillary Clinton kutaka kuanguka baada ya kuugua ghafla, mwanasiasa huyo ameibuka na kusema  hakutaka kuweka wazi kuhusu ugonjwa huo kwa kuwa hakudhani ni wa kutisha.
Clinton ambaye ni mgombea wa urais wa Chama cha Democratic alitaka kuanguka wakati alipohudhuria kumbukumbu ya shambulio la Septemba 11 nchini humo.

Akihojiwa na shirika la habari la CNN, Clinton amesema kuwa hakufuata vyema kile anachokiita ushauri wa madaktari wake wa kupumzika kwa siku tano baada ya kufanyiwa vipimo siku ya Ijumaa.

Timu yake ya kampeni imesema kuwa hana tatizo lolote la kiafya isipokuwa homa ya mapafu na kuongeza kuwa taarifa zaidi juu ya uimara wa afya yake zitatolewa.

Mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump,amesema kuwa anatumai Clinton atapona hivi karibuni,na kuongeza kuwa ugonjwa wa mgombea huyo ni tatizo katika mbio za urais.
Kwa upande wake, Trump amesema kuwa ofisi yake itatoa taarifa yake ya kiafya wiki hii.

No comments:

Post a Comment