M
rembo wa taji la Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza
na wageni walikwa pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
wa uzinduzi wa duka lake la samani za ndani “Amorette” lililopo katika
jengo la Village Walk gorofa ya kwanza karibu na Sea Cliff Hotel, Masaki
jijini Dar es Salaam.
Bi. Jacqueline Mengi akikata utepe kuzindua duka lake hilo.
Ha ha ha ha, sasa mko huru kuingia wageni waalikwa kujionea
yaliyomo,…..Bi. Jacqueline Mengi akifurahi jambo mara baada ya kukata
utepe.
Bi. Jacqueline Mengi akiongozana na baadhi ya wageni waalikwa kuingia ndani ya duka la “Amorette”
Balozi Juma Mwapachu na baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia moja ya
meza ya chakula (dining table) iliyotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga
baada ya kuzinduliwa duka hilo lililopo katika jengo la Village Walk,
Masaki jijini Dar.
Wageni waalikwa wakiendelea kukagua samani mbalimbali katika duka hilo.
Mmoja wa wageni waalikwa akitazama bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga ndani ya duka la Amorette.
Baadhi ya samani zilizomo ndani ya duka la Amorette.
Wageni waalika wakiangalia moja ya kitanda cha aina yake kinachouzwa
katika duka la Amorette lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki
jijini Dar es Salaam.
Bi. Jacqueline Mengi akizungumza jambo na Balozi Juma Mwapachu wakati
akiwatembeza wageni waalikwa katika maeneo mbalimbali ndani ya duka lake
la Amorette.
Wageni waalikwa wakiendelea kutazama kitanda hicho cha aina yake.
Sehemu maalum ya kitanda hicho ya kuhifadhia mashuka, Blanket pamoja na mito.
Wanahabari na wageni waalikwa wakiwa ndani ya duka la Amorette kujionea bidhaa mbalimbali.
Bi. Jacqueline Mengi akipozi katika moja ya samani ndani ya duka lake la Amorette.
Balozi Juma Mwapachu (kushoto) akibadilishana mawazo na mwalikwa mwenzake kwenye uzinduzi wa duka la Amorette.
Mwanadada Monica Joseph akipozi kwenye moja ya bidhaa zilizopo ndani ya duka la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi katika pozi matata ndani ya duka lake la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua duka lake la samani za ndani la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akipozi kwenye samani moja wapo inayopatikana katika duka lake la Amorette.
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo ndani ya duka la Molocaho-Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akiwa kwenye picha ya pamoja na rafiki zake.
Warembo wakiwa wamepozi kwenye samani zinazopatikana katika duka la
Amorette lililopo ndani ya jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa Dorice Mollel Foundation, Dorice Mollel (kulia) katika picha ya pamoja na Mdau Monica Joseph.
So
phia Byanaku akijinafasi katika moja ya samani zilizomo kwenye duka la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akibadilishana mawazo na baadhi ya marafiki zake.
Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na Dorice Mollel.
katika historia ya
mjasiriamali, Jacqueline Mengi kwa kufanya uzinduzi wa duka la samani za
ndani la Molocaho Amorette likiwa na vitu ambavyo ni vya pekee kutokana
na aina ya malighafi ambayo wametumia kutengeneza.
Akizungumzia duka hilo, Bi.Mengi alisema kuwa ilikuwa ni ndoto yake ya
muda mrefu ya kutaka siku moja kuwa na duka kama hilo ambalo litakuwa na
samani ambazo ni ngumu kuzipata sehemu nyingine kutokana na
kutengenezwa tofauti na samani nyingi ambazo zinapatikana madukani.
“Siamini kama ndoto yangu imetia, kwa kipindi cha miaka iliyopita kuna
vitu nilikuwa nikitamani kuwa navyo nyumbani lakini sikuweza kuvipata
nilipokuwa nikitafuta na hapo ndipo ndoto za kuwa na duka zilipoanzia,
“Nilikuwa nataka kitu cha tofauti ambacho ni ngumu kukikuta sehemu
nyingine kutokana na kuwa na ubunifu wa kipekee ambao utawavutia wateja
wa ndani ya nchi na nje ya nchi na ninaamini watafurahia,” alisema Bi.
Mengi.
Aidha Bi. Mengi alisema kuwa bidhaa ambazo zitakuwa zikipatikana katika
duka la Molocaho – Amorette zimetengenezwa na malighafi kutoka Tanzania
kama mbao za Mninga na hivyo kuwataka Watanzania kuwa wazalendo kwa
kutumia bidaa ambayo imetengenezwa na malighafi za Tanzania.
Mmoja wa wageni waliohudhuria halfa ya uzinduzi, Faraja Nyalandu alisema
kuwa kwa kijana kama Jacqueline Mengi kuwa na duka kama hilo ni hatua
kubwa ambayo vijana wengi wanatamani kuifikia, kumpongeza kwa juhudi
alizozifanya lakini pia kutoa ushauri kwa wengine ambao wanataka
kufanikiwa.
“Kwanza nimpongeze Jacqueline amefanya uthubutu na amefanikiwa kuwa na
kitu kama hiki, juhudi yake inaonyesha kuwa kila mtu tu anaweza
kufanikiwa kama akiongeza juhudi katika jambo analotaka kulifanya,”
alisema Bi. Nyalandu.
Duka hilo la kisasa na la aina yake linapatikana Masaki karibu na hoteli
ya Sea Cliff kwenye jengo la “Village Walk” gorofa ya kwanza.
No comments:
Post a Comment