Sunday, 4 September 2016

Balozi wa Marekani UN ataka wabakaji Sudan Kusini kukamatwa

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, ameiomba serikali ya Sudan Kusini kuwakamata na kuwachukulia sheria watu waliokuwa na silaha ambao waliwabaka na kuwapiga wanawake wa kigeni katika hoteli moja nchini humo mwezi Julai mwaka huu.
Watu hao pia walimpiga risasi na kumuua mwaandishi habari mmoja wa Sudan Kusini.

Samantha Power, amesema hayo alipofanya ziara ya kipekee nchini humo, ziara iliyoandaliwa na baraza la usalama la Umoja wa mataifa, ambalo limeomba utawala wa Sudan Kusini kufutilia mbali ugumu wake, wa kuwakubalia walinda usalama wa Umoja wa Mataifa kuingia nchini humo.

Hayo ni baada ya kutokea mapigano kati ya wanajeshi wanamotii Rais Salva Kiir na wale wa aliyekuwa makamu wa Rais Daktari Riek Machar.

Makabiliano hayo yalifanyika mjini Juba, likiwemo shambulio hilo kwenye hoteli, ambalo kidole cha lawama kimenyoshewa wanajeshi wa serikali.

No comments:

Post a Comment