Kamati ya kimataifa ya Olimpiki – IOC imezindua timu yake ya kwanza
kabisa ya wakimbizi itakayokuwa na wanamichezo 10 na maafisa 12 na
itashindana katika Michezo ya Olimpiki ya Rio 2016 chini ya bendera ya
Olimpiki
Bach amesema "Tuna hakika kuwa timu hii ya wakimbizi katika Olimpiki inaweza kuwa idhara ya matumaini. Ishara ya matumaini kwa wakimbizi wote ulimwenguni na inaweza kutuma ujumbe kwa jamii ya kimataifa kuwa wakimbizi ni binadamu wenzetu na muhimu katika jamii. Wanamichezo hawa wakimbizi wataonyesha ulimwengu kuwa licha ya mikasa mikubwa waliyopitia, yeyote anaweza kuchangia katika jamii kupitia vipaji vyao, ujuzi na nguvu za roho ya kibinaadamu"
IOC itaipa timu hiyo ya wakimbizi sare za michezo na kuwapa makocha na maafisa wa timu
No comments:
Post a Comment