Mgombea anayepewa nafasi kubwa ya
kupeperusha bendera ya Republican katika kinyanganyiro cha urais huko
Marekani Donald Trump amesema muda umefika kwa nchi hiyo kutafakari kwa
kina juu ya matumizi ya taarifa binafsi za watu katika harakati za
kupambana na uhalifu.
Bwana Trump aliyasema hayo katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha habari za CBS akijaliana juu ya mpango wa siku za usoni wa taifa hilo,kufuatia mauaji yanayokithiri nchini humo, na hasa la hivi karibuni katika klabu moja ya usiku mjini Orlando yaliyojiri wiki iliyopita.
Ameongeza kusema kwamba nchi zingine zimetumia mbinu tata za rangi ya mtu , dini, utaifa au ukabila kama mbinu ya kutambua nani anaweza kufanya uhalifu.
No comments:
Post a Comment