Tuesday 29 March 2016

Waliokata Tiketi Kurudishiwa Fedha Zao

bShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwarudishia fedha zao kesho Jumanne, wapenzi Wa mpira wa miguu waliokuwa wameshakata tiketi za kushuhudia mchezo wa kundi G kati ya Tanzania v Chad jijini Dar es salaam.

TFF inawaomba washabiki wa mpira wa miguu waliokua wamekata tiketi za mchezo huo, kufika kesho Jumanne saa 5 kamili asubuhi katika vituo walivyonunulia wakiwa na tiketi zao ili waweze kurudishiwa fedha zao.

Zoezi la kuwarudishia fedha washabiki waliokuwa wameshakata tiketi za mchezo kati ya Tanzania v Chad litafanyika katika vituo vinne vilivyokua vikiuza tiketi siku ya Jumapili, hivyo wenye tiketi za mchezo huo wanaombwa kufika na tiketi zao ili waweza kurudishiwa fedha zao.

Aidha TFF inawaomba radhi watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu uliojitokeza Na kuwataka kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki ambacho Wanasubiria Taarifa zaidi kutoka CAF.
Chad imejiondoa jana katika kinyanganyiro cha kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) nchini Gabon mwaka 2017, ambapo iliku kundi G na timu za Misri, Nigeria Pamoja na Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu  Wa MamlakaYa Usafiri Wa Anga Kuwait Mhandisi Yousef Al  Fozan Awasili  Nchini  Kusaini Makubaliano  Ya Usafiri  Wa Anga  Na TCAA.

A5Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan , maoja na Msafara wake Wakiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es alaam leo.
A4Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari, (wapili kushoto)  akiwa na maofisa wa Ubalozi wa Kuwait hapa nchini kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es alaam  wakimsubiria Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan aliyewasili nchini kwa ajili ya kusaini makubaliano ya safari za Anga baina ya Tanzania na Kuwait.
A1Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari (Kushoto)akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait  ,Mhandisi Yousef Al Fozan ,mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo,Kwa ajili ya kusaini  makubaliano ya safari za Anga baina ya Tanzania na Kuwait.
A3Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari, (wapili kushoto)  akiwa kwenye gari pamoja na wageni wake kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Ya Usafiri wa Anga Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan na Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Ubalozi Wa Kuwait Nchini, Mohamed Rashid Alamiri, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege Wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es alaam leo,Kwa ajili ya kusaini makubaliano ya safari za Anga baina ya Tanzania na Kuwait.
indexMkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari,  (wapili kushoto)  akiwa na mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan, wakati alipowasili kwenye  uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es alaam kwa ajili ya kusaini makubaliano ya safari za Anga baina ya Tanzania na Kuwait.
A2 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan ,(Kulia) Akimfafanulia jambo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania,(TCAA) Hamza Johari, kuhusiana na usafiri wa Anga mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es alaam leo,Kwa ajili ya kusaini makubaliano ya Safari za Anga baina ya Tanzania na Kuwait.

No comments:

Post a Comment