Thursday 17 March 2016

Asdimamishwa kwa kumdanganya Waziri mkuu Kassim Majaliwa

JIL
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Chato, Bw. Peter Ngunura kwa kosa la kumdanganya mbele za watu na kumpa taarifa za uongo juu ya pampu ya maji iliyodaiwa kupelekwa Morogoro.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Machi 16, 2016) alipokuwa akiwahutubia Mamia ya wakazi wa mji wa Chato waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wilayani Chato, mkoani Geita.
 
Waziri Mkuu ambaye amewasili mkoani Geita kwa ziara ya siku mbili akitokea mkoani Kagera, Alisimamishwa na wakazi wa kijiji cha Kalebezo, kata ya Nyamirembe, wilayani Chato na kukuta mabango yaliyokuwa yakidai maji safi na kuelezea uharibifu wa pampu ya maji.
 
Katika maelezo yao, wakazi hao walimweleza Waziri Mkuu kwamba mradi wa maji kwenye kata Hiyo ulishakamilika lakini pampu yao imechukuliwa na kupelekwa Morogoro jambo lililosababisha wakose maji kwa muda mrefu.
 
Kwa sababu alikuwa hajafika Chato mjini na hakuwa na taarifa sahihi za mradi huo wa maji, Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi hao kwamba analibeba jambo hilo na atafuatilia hadi aelezwe ni kwa nini pampu hiyo imepelekwa Morogoro.
Akiwa kwenye mkutano wa hadhara, ndipo suala la maji likaibuka tena na Waziri Mkuu kuamua kuchukua hatua hiyo.
 
“It’s unethical (ni kinyume cha maadili) kumdanganya kiongozi wako. Nimekuuliza mara mbili Mbili kama una uhakika kuwa pampu hiyo ipo ukasema una uhakika kuwa ipo. Nimemtuma Diwani na vijana wangu wakacheki wakasema hakuna pampu,” alisema Waziri Mkuu na kumwita Diwani huyo jukwaani ili atoe majibu.
 
“Pale kulikuwa na pampu mbili; moja ni ya kuvuta maji kutoka kwenye kina kirefu na kuyapeleka kwenye pump house na nyingine ni ya kuvuta maji kutoka kwenye pump house na kuyapeleka kwenye tenki kubwa la kuhifadhia maji. Ile ya kutoa maji kwenye kina kirefu ndiyo haipo, wataalamu wanajua wameipeleka wapi,” alisema Bw. Charles Manoni ambaye ni diwani wa kata ya Nyamirembe ambayo kijiji cha Kalebezo kimo.




No comments:

Post a Comment