Monday 21 March 2016

Mbunge wa Jimbo la Kibiti awavalia Njuga Watumishi Wazembe Wanaofanya kazi kwa Mazoea

ruf1
Mbunge wa Jimbo la Kibiti  Ally Ungando akiwaonyesha wananchi cheti maalumu cha pongezi alichopatiwa na Chama cha walemavu kwa ajili mchango wake mkubwa katika kuisaidia jamii  kushoto kwake ni Katibu wa chama cha waemavu Kibati Selemani Zalala,

Na Chrispino Mpinge
MBUNGE  wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando amewataka watendaji na viongozi kutokuwa wazembe Na  kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawajibike ipasavyo kuwatumikia wananachi wao ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika kukuza maenedeleo.
 
Kauli hiyo ameitoa katika mkutano wa hadhara  na wananchi wa kata ya Bungu ulioandaliwa kwa lengo la kuweza kuwashukuru kwa kuweza  kumpatia nafasi ya kuwaongoza kwa kipindi cha  Miaka mitano ambapo ulihuiwa wa na viongozi wa serikali pamoja na watendaji wa kijiji,kata pamoja na Wilaya.
 
Ungando alisema  kwamba serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuleta mabadiliko hivyo kwa upande wake hawezi kuwavumilia wale wote ambao watabainika wanafanya kazi kwa kuangalia  maslahi yao binafsi bila kuangalia  vipaumbele wanavyovihitaji wananchi hao.
 
Aidha Mbunge huyo amebainisha kwamba baadhi huduma  za kijamii ambazo zilikuwa zimekwama ikiwemo afya,elimu,vyoo  pamoja na mambo mengine  kutokana na  kuwepo kwa utendaji mbovu ameahidi kuzitatua haraka iwezekanavyo iii wananchi waweze kuondokana na kero hizo.
Pia  Mbunge huyo wa  Jimbo la Kibiti  ameahidi kutoa mabati 100 kufanikisha ujenzi wa shule ya msingi Kibwibwi kuwawezesha wanafunzi kupata huduma ya elimu karibu na wanapoishi.
 
Ungando alisema, bati hizo zitatokana na fedha za mfuko wa jimbo, lengo likiwa ni kutatua changamoto zinazokwamisha maendeleo katika jimbo hilo.
 
Aidha aliwaomba wananchi kudumisha ushirikiano kufanikisha kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jimbo la kibiti ikiwemo kuepusha migongano ambayo inadumaza maendeleo.
 
Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata ya Bungu Mohamed Mketo alisema asilimia kubwa ya Watoto wanaoishi katika kitongoji cha Kibwibwi wanashindwa kuendelea na masomo kutokana na umbali mrefu.
 
 Nao baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo   hawakusita kutoa kilio chao kinachowakabili akiwemo Salum Kasuku,Salum Pazi,pamoja na Asia Mohamed walisema Wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo huduma ya  afya, ukosefu wa  maji safi na salama  pamoja na kukabiliwa na uhaba wa wauguzi pamoja na madaktari.
 
Kwa upande wake Diwani wa kata ya bungu Ramadhani Mpendu akijibu baadhi ya malalamiko Yaliyotolewa na wananchi hao katika mkutano huo  amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.

No comments:

Post a Comment