Wednesday 30 March 2016

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhandisi Hamad Masauni amefanya Ziara Mkoani Kigoma Katika Kambi ya Wakimbizi


D1Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akisalimiana na Wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa yanayohudumia wakimbizi katika Kambi ya muda ya NMC, iliyoko mkoani Kigoma, kushoto ni Mratibu wa Wakimbizi  Mkoani  Kigoma, Tonny  Samwel  Laiser.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
D7Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wakimbizi wa Burundi (hawapo pichani) wanaoishi katika kambi ya Mtendeli, iliyoko wilayani Kakonko mkoani Kigoma.Naibu Waziri yuko Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
D2Msimamizi  wa  Kambi ya muda ya NMC, Jordan Emmanuel (wa kwanza kushoto), akimuonyesha Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, jinsi mfumo wa jiko la kupikia chakula  kambini hapo unavyofanya kazi.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
D3Sehemu ya vitanda vipya vikiwa katika moja ya mabweni ya Kambi ya muda ya wakimbizi ya NMC , tayari kwa kufungwa na kuanza kutumika na wakimbizi wanaohifadhiwa kambini hapo.
D4Naibu Waziri wa Wizara  ya  Mambo ya Ndani  ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akizungumza na  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani  Kigoma, Peter Toima Kiroya (wa kwanza kushoto), wakati  walipotembelea  iliyokua kambi ya Karago iliyotumika kuhifadhi wakimbizi.Kulia ni Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Mtendeli, Innocent Mwaka.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
D5Naibu Waziri wa Wizara  ya  Mambo ya Ndani  ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani Ofisi ndogo ya Kibondo, Dost Yousafzai(kushoto), wakati alipotembelea iliyokuwa kambi ya Wakimbizi ya Karago,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Serikali YAJIPANGA KUWASAIDIA WAKULIMA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHi

DSC_1667
Wageni rasmi katika mkutano huo, Wa kwanza kushoto ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN), Njongenhle Nyoni, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai.
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha inawasaidia wakulima kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanaonekana kuendelea kuikabili nchi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) na Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN) ili kujadili mpango wa Kilimo Salama (CSA).
Bi. Natai alisema serikali inatambua uwepo wa mabadiliko ya Tabia ya Nchi na kwasasa tayari wataalamu Wanafanya tafiti ili waone ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia wakulima kupambana na mabadiliko hayo.
Alisema kwa sasa bado wakulima wengi hawajafahamu kama kuna mabadiliko ya tabia ya nchi na hivyo Wamekuwa wakitumia njia za asili lakini baada ya utafiti watapatiwa mbinu mpya za kupambana na mabadiliko ambapo wataweza kutumia njia za kisasa ambazo zinaonekana kuwa bora zaidi.
“Serikali inatambua na tunajipanga kuwasaidia wakulima, shida kwa sasa bado wakulima wengi hawajajua kama kuna mabadiliko ya tabia ya nchi lakini wataalamu wapo wanafanya tafiti baada ya hapo tutajua tunawasaidia vipi,
“Kwa sasa kinachoonekana ni kutokueleweka kwa hali ya hewa kama mafuriko kutokea lakini kwa kuwa bado hawajapatiwa elimu wanashindwa kutambua na bado wanatumia njia za asili, tutawapa mbinu mpya watafanya kwa pamoja na mbinu wanazotumia sasa za asili,” alisema Bi. Natai.
Aidha alieleza kuwa baadhi ya huduma ambazo watapatiwa wakulima baada ya kukamilika kwa tafiti ni pamoja na kupewa elimu ya kilimo cha umwagiliaji, mbegu za kisasa ambazo zinawahi kukomaa na dawa za kupambana na magonjwa.
Nae mtafiti kutoka FANRPAN, Njongenhle Nyoni alisema taasisi yake imefanya mkutano huo ili kuona ni jinsi gani Wanaweza kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi katika nchi ambazo wanafanya kazi ambapo Tanzania ni mojawapo.
Alisema wao wanafanya tafiti kuona hali ilivyo na baada ya hapo wanatazama changamoto zilizopo katika kupambana na mabadiliko na wanatoa ushauri ni jambo gani linaweza kufanyika ili kuwezesha kufanikisha kufanyika Kilimo Salama (CSA).
“Tunakutana na watu kutoka asasi za kijamii na taasisi mbalimbali ili kuona ni jinsi gani CSA inaweza kufanya kazi Vizuri hasa katika maeneo tunafanya nao kazi na hii sio Tanzania tu hata mataifa mengine kama Malawi tunalifanya hili,” alisema Nyoni.
Pia iliongeza kuwa malengo ya FANRPAN ni kusaidia wakulima kuondoka katika janga la umasikini lakini pia kuwepo kwa chakula kilicho katika hali ya usalama bila kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.
DSC_1671Baadhi ya wageni waliohudhuria katika mkutano huo kujadili mpango wa Kilimo Salama (CSA).
DSC_1682Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi.
DSC_1697
DSC_1701
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai akielezea Kilimo Salama (CSA).
DSC_1749
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuendelea na mkutano huo.
DSC_1754
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai.
DSC_1759
Karl Deering kutoka Taasisi ya CARE akizungumzia Mpango wa Kilimo Salama Afrika (ACSAA)
DSC_1769
Baadhi ya wageni katika mkutano huo wakichangia hoja
DSC_1772
DSC_1819
Washiriki wa mkutano wakiwa katika makundi kujadili kuhusu Kilimo Salama (CSA)
DSC_1823
DSC_1829
DSC_1914
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uwezeshaji wa ESRF, Doris Likwelile akifunga mkutano.

No comments:

Post a Comment