Monday 28 March 2016

Rais John Magufuli apokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibibiti wa Serikali CAG Ikulu Dar es salaam


J1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
J4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakipitia Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali iliyokabidhiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
J2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakiwa na watendaji wakuu  wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkafuzi Mkuu wa Hesabu za serikali  baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
PICHA NA IKULU
C3Kocha wa TSS, Michael Livingstone akiwafundisha  waogeaji Celina Itatiro na Marin de Villard kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg Afrika Kusini kwa ajili ya Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South Africa level 2
C4Kocha wa TSS, Alex Mwaipasi akiwafundisha waogeaji wa TSS, kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg Afrika Kusini kwa ajili ya Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South Africa level 2
C5Adil Bharmal na Pieter De Raadt wakionyesha ufundi wao katika ku-dive wakati wa mazoezi ya timu ya TSS kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park kabla ya mashindano ya South Africa level 2
C2Waogeleaji wa Tanzania Swim Squad (TFF) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg Afrika Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South Africa level 2
C1
C6Viongozi wa timu ya Tanzania Swim Squad (TSS), Thauriya Diria (wa kwanza kushoto) na Inviolata Itatiro (Katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na kocha  Michael Livingstone wakiwa katika picha ya pamoja TSS kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park kabla ya mashindano ya South Africa level 2

Na Mwandishi wetu,
Jumla ya waogelaji nane wa timu ya Tanzania Swim Squad (TSS) watakuwa na ratiba ngumu kesho ya kuwania medali mbalimbali katika siku ya pili ya mashindano ya Kimataifa ya Afrika Kusini “South Africa Level 2” yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park.
Waogeleaji hao ni Celina Itatiro, Marin de Villard,  Adil Bharmal, Amani Dogart, Josephine Oosterhuis, Jacquelene Kortland,  Isabella Kortland, Pieter De Raadt, Celina Itatiro na Marin de Villard.
Waogeleaji hao  watawania medali katika mashindano ya mita 50, 100, 200 na relay katika kwa upande wa wanawake na wanaume  kwa kushindana na waogeeaji wengine kutoka nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Namibia na wenyeji Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa  na waandaaji, Adil ndiye ataanza kuwania medali kwa uande wa Tanzania kwa waogeaji wenye umri  miaka 16  na kufuatiwa na Marin kwa upande wa mita 200 freestyle kwa waogeleaji wa wa Miaka 11 na baadaye wasichana, Celina na Amani kushindana kwa upande wa wanawake wenye umri wa miaka 11 katika staili ya free style.

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Adil na Marin wataingia tena kwenye ‘maji’ kushindana katika staili ya breaststroke Mita 100 kwa upande wa umri wao ns baadaye Josephine na Jacqueline watapambana kwa watoto wenye umri wa miaka 15 na kufuatiwa na Celina na Amani tena.
Baada ya kushindana katika staili hizo mbili (freestyle na breaststroke mita 100 na 200), waogealeaji, Adil na Marin wataingia tena mashindananoni kuwania medali kwa upende wa mita 50 backstroke na baadaye Isabela Kortland, Josephine, Amani na Celina watawania medali tena.

“Ni ratiba ngumu sana kwa waoageaji wetu, ila tunashukuru kuwa wameweza kufanya mazoezi na kidogo kuzoea Hali ya hewa ya ubaridi, sisi (TSS) tutatokea mji wa joto inaweza kutupa shida kwani baridi ya huku inaambatana na jua la kuchoma, si hai nzuri, ila tutajitahidi,” alisema Alex Mwaipasi.
Mwaipasi ambaye yupo na kocha mwenzake, Michael Livingstone alisema kuwa mashindai hayo ni magumu sana kutokana na idadi ya waogeleaji na idadi ya mashindano ambayo kila muogeleaji atashindana.
“Celina anatarajia kushindana katika mashindano tofauti 11, si mchezo na waogeleaji wpo zaidi ya 1000, nchi nyingi za ukanda wa Kusini mwa Afrika wameleta waogeaji, ni mashindano mazuri kwa kuwapa uzoefu waogeleaji wetu,” alisema Michael.

No comments:

Post a Comment