Friday 25 March 2016

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Stephan P Masatu kuendesha Huduma ya Uchunguzi wa Maradhi ya Moyo Mkoani Kigoma


DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo, Dkt. Stephan P. Masatu
 Na Mwamvita Mtanda
WATU wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo mkoani Kigoma, watapata faraja kubwa mapema Aprili 4 hadi 9, 2016, kufuatia uwepo wa huduma za uchunguzi wa maradhi hayo utakaofanywa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo, Dkt. Stephan P. Masatu, kutoka jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam, Dkt. Masatu alisema, huduma zote za magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na vipimo vya ECG na ECHO zitatolewa kuanzia asubuhi kwenye hospitali ya kibinafsi ya Upendo iliyo jirani na soko kuu la mkoani Kigoma.
Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi na zinakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa kushughulikia magonjwa kama ya Moyo na kutokana na uchache wa wataalamu hao, itakuwa ni nafasi nzuri kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na vitongoji vyake, kujitokeza ili kuhudumiwa ambapo kliniki hiyo itadumu kwa muda wa siku sita mfululizo.
Dkt. Masatu akitumia mashine ya kupima ECHO, mmoja wa wagonjwa wa moyo

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwako na ongezeko la Maji
katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, pamoja na maeneo ya miji ya
Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya mtambo wa Maji wa Ruvu chini kuanza
kufanya majaribio ya uzalishaji wa Maji .
Akiongea na waandishi wa habari kaimu meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amesema kuwa
kutokana na ongezeko hilo la Maji watu wengi wameanza kupata huduma ya
Majisafi, na pia kumekuwepo na ongezeko la uvujaji wa Maji katika maeneo mengi
ya jiji la Dar es salaam, hasa katika maeneo ambayo yalikuwa na miundombinu ya
Maji lakini hayakuwa na huduma ya Maji na baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa yakipata
Maji kwa msukumo mdogo (Low pressure)

Kufuatia ongezeko hili la Maji watu wengi wameanza kupata huduma ya Majisafi, na uvujaji
wa Maji umeongezeka katika maeneo ambayo aidha yalikuwa na miundombinu ya Maji
lakini hayakuwa na huduma ya Maji au maeneo ambayo yalikuwa yakipata Maji kwa
msukumo mdogo” Alisema Bi. Lyaro

Aidha, ametoa wito kwa wateja na wananchi wote kutoa taarifa za uvujaji huo wa Maji pindi
wanapobaini kuwapo na uvujaji wa Maji katika makazi yao na maeneo mbalimbali ya
jiji kupitia kituo cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 022194800 au
0800110064 (Bure).
“Namba hizi ziko wazi saa 24 kwa siku na mteja hatakatwa gharama yoyote akipiga simu hizi. Hivyo
tunaomba wateja wetu waisaidie Dawasco kupunguza upotevu wa maji kwa kutupa
taarifa za mivujo na kupasuka kwa mabomba” alisema bi Lyaro.
Kutokana na ongezeko hilo la Maji maeneo yaliyoanza kupata Maji baada ya majaribio ya mtambo huo
kuwa ni Tandale,Manzese makunimula,Mwananyamala,Kinondoni mkwajuni, baadhi ya
maeneo ya vingunguti,changombe,ubungo-mabibo na city centre.
Pia, DAWASCO imetumia nafasi hiyo kuwakumbusha wateja wote kulipia huduma ya Maji kwa wakati kwani
watu wengi kwa sasa wameanza kupata huduma ya Majisafi na salama kutokana na
kuongezeka kwa uzalishaji wa Maji katika mtambo wa Maji wa Ruvu chini, hivyo
hawana budi kuyalipia ili kuepuka usumbufu wa kusitishiwa huduma ya Maji.
Kuongezeka kwa huduma ya Maji katika jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo  kumetokana na kukamilika upanuzi wa mtambo wa
Ruvu chini ulioanza mwaka 2011 hivyo kuongezeka kiasi cha uzalishaji wa Maji
kutoka wastani wa lita milioni 182 hadi lita 270 kwa sasa.

WANAFUNZI WA FEZA BOYS HIGH SCHOOL WATEMBELEA VIRGINIA INTERNATIONAL UNIVERSITY

Wanafunzi wa Feza Boys High School kutoka jijini Dar es Salaam wakipata picha ya pamoja walipokua Virginia International University iliyopo jimbo la Virginia siku ya Alhamisi March 24, 2016, wanafunzi hao wapo kwa ziara maalum ya kuangalia uwezekano wa kujiunga na chuo hicho katika masomo ya juu.
 Makamu Rais wa Chuo hicho Dr. Suleyman Bahceci (kulia) akiwaeleza wanafunzi hao taratibu za kufuata kwa ajili ya kujiunga na VIU
Kushoto ni Alex Luketa Mtanzania anayefanyakazi chuoni hapo kwa ajili ya kusajili wanafunzi kutoka Afrika Mashariki akiwa pamoja na wanafunzi wa Feza Boys High School wakimsikiliza Makamu Rais wa chuo (hayupo pichani) alipokua akielezea wanafunzi hao utaratibu wa kujiunga na masomo VIU.
Wanafunzi wa Feza Boys wakipata mulo.
Mazungumuzo yakiendelea.
 Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment