Monday 21 March 2016

Kichawa yazindua Mfumo Shirikishi kwa Bodaboda

indexNa Kalonga Kasati

Uongozi wa kampuni ya Kikundi cha Waadhirika wa Maendeleo (KICHAWA) unaojishughulisha na Usafirishaji wa mizigo wamezindua mwongozo wa  mfumo shirikishi wa uratibu wa Bodaboda na Bajaji nchini.

Akizindua mfumo huo leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Mussa Chengulla na kusema kuwa lengo ni kupambana na kupata suluhiso la kudumu katika sekta ya Usafirishaji wa Bodaboda na Bajaji juu ya changamoto za kisheria, kiusalama na 

kimazingira.Chengulla amesema kuwa sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa mfumo huo ni Matokeo makubwa ya changamoto zilizojitokeza katika jamii juu ya wizi wa pikipiki, wizi wa kutumia pikipiki, uvunjifu wa sheria za usalama barabarani, kanuni za usafirishaji, matumizi ya Kujichukulia sheria mkononi, uegeshaji holela wa bodaboda na bajaji na ukamataji usio salama.

 “Uwanzishwaji wa mfumo huu shirikishi ni kukabiliana na changamoto zitokanazo katika sekta ya  Usafirishaji na kutatua kero hatarishi zinazoikabili jamii ili kufika malengo ya kuiondoa ajira ya Bodaboda na bajaji katika orodha ya ajira hatarishi, kero na janga la Taifa na kuifanya kuwa ajira Tegemezi, endelevu na salama kwa usalama wa raia na mali zao” aliongeza Bw. Chengulla.

Mbali na hayo Bw. Chengulla amesema kuwa watakaonufaika na mfumo shirikishi ni TAMISEMI Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya kwa kutambua idadi kamili ya wanaoendelea kujiajiri na kuajiriwa kupitia sekta ya Usafirishaji abiria.

Pia Wengine watakaonufaika na mfumo huo shirikishi ni SUMATRA, Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Jeshi la Polisi na Usalama ya Raia na kitengo cha usalama barabarani, wamiliki na Madereva wa bodaboda na bajaji kulingana na kazi za  sekta husika.

No comments:

Post a Comment