Tuesday 29 March 2016

Sumatra kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani Wafanikiwa Kukamata Mabasi 105

3Meneja Mawasiliano wa  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) bw. David Mziray  akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu kukamatwa kwa mabasi Yaliyobainika kukiuka masharti ya Leseni  nyakati za asubuhi na jioni katika jiji la Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO bw. Frank Mvungi.
4Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano  wa  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga kuhamasisha wadau wa Sekta hiyo kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta hiyo.


Kalonga Kasati

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,Kikosi cha Usalama Barabarani wamefanya ukaguzi katika Jiji la Dar es salaam,ambapo Wamefanikiwa kukamata mabasi  105 na kati hayo 36 yamefikishwa mahakamani  baada ya  kukiuka wa masharti ya leseni ya usafirishaji abiria.

Hayo yamwebainishwa leo  na Meneja Mawasiliano wa SUMATRA Bw. David Mziray wakati wa Mkutano na vyombo vya habari uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo katika kutatua kero zinazowakabili abiria nyakati za asubuhi na Jioni.

Akifafanua Mziray amesema kati ya Machi 21-24 , 2016  ilifanya ukaguzi huo  na ili sheria iweze kuchukua mkondo wake Kwa wale wanaokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.

“Katika kuimarisha huduma za usafiri Mamlaka  imeweka utaratibu maalum wa kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo katikati ya jiji,Ubungo,Buguruni na Kariakoo ili kubaini wale wote wanaovunja sheria”.alisisistiza Mziray.

Akizungumzia baadhi ya makosa yalibainika kutendwa na mabasi hayo Mziray alisema kuwa ni Pamoja na kuongeza nauli,kukata njia,kutoa huduma bila leseni ya usafirishaji,kutoa huduma katika njia ambazo hawakupangiwa.

Wamiliki na wafanyakazi katika sekta ya usafirishaji kote nchini  hasa wa mabasi ya daladala Wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji wanapotoa huduma hiyo kwa umma.

Mziray  aliongeza kwamba  wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale Wanapobaini  basi walilopanda linakiuka masharti ya leseni ikiwemo kuongeza nauli,kukata Njia,kutoa huduma bila leseni ya usafirishaji na kutoa huduma katika njia ambazo hawakupangiwa Ambapo wananchi wanaweza kutoa taarifa kupitia namba za simu za bure ambazo ni 0800110019 na 0800110020.

No comments:

Post a Comment