Thursday 24 March 2016

Ritha Kabati Ccm Kutoka Mkoa wa Iringa arudi Bungeni


rita
Na Kalonga kasati 
WABUNGE wa Viti Maalum watatu Wameingia baada ya uchaguzi majimbo Yote  kukamilika ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata viti maalum viwili na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mmoja.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu ,Damian Lubuva amesema kuwa  uchaguzi umekamilika katika majimbo nane kwa kuwa na majimbo ya Tanzania Bara saba na Zanzibar Moja ambalo ni Jimbo la Kitope Upele.
Viti vya wabunge wa viti maalum wanatokana na kura za jumla za wabunge wote na kuweza kupatikana viti hivyo.
Waliopatikana katika mchanganuo wa viti maalum ni, Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema).
Lubuva amesema kuwa kufikia hapo ndipo uchaguzi umekamilika kutokana na viti hiyo kupatikana na kufanya kuwa viti maalumu 113 katika mgawanyo wa viti hivyo ni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Viti  66,  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  viti 35 pamoja na Chama cha Wananchi (CUF)  viti 10.
Amesema kuwa kutokana na chaguzi zinazoendelea NEC ndiwe iwe sehemu ya usimamizi wa chaguzi zote.
Idadi kura za wabunge CCM katika uchaguzi ambazo zilibaki kutokana wagombea kufariki na kuarishwa kumeongeza viti maalum viwili.

No comments:

Post a Comment