Mjumbe wa Serikali za Mtaa wa
Mikocheni B, Kamati ya Mazingira Moses Sanga pamoja na Victoria Kileo wa
Nipe Fagio wakiwa wamebeba taka wakati wa zoezi la kufanya usafi katika
fukwe za Mbezi Beach leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo
limeshirikisha Marafiki wa Bahari, Nipe Fagio,Mbezi Beach Neighborhoods.
Delicia Mwanyika and Cindy
Tibazarwa kutoka Mbezi beach Neighborhoods wakishilikiana kuokota taka
sugu kama vile Plastiki, makopo, nguo, viatu, nyavu, mataili, sindano,
vyupa na taka nyingi zaidi.
Beatrice Steyn Muasisi wa Mbezi
Beach Neighborhoods akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi
la kufanya usafi wa fukwe ya Mbezi Beach katika kuokoa Bahari ambapo
alisisitiza ushirikiano kutoka Serikali, Viwanda, Taasisi mbalimbali
pamoja na watu binafsi kuungana kwa pamoja kurudisha uhai wa bahari
ambayo inaelekea kufa kama hakuna hatua itakayo chukuliwa sasa.
Boss Brown Muasisi wa Marafiki wa
Bahari kutoka Mikocheni B akiwa katika zoezi la kufanya usafi katika
fukwe za Mbezi Beach leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshirikisha
Marafiki wa Bahari, Nipe Fagio,Mbezi Beach Neighborhoods.
Washiriki wa zoezi la usafi wa
fukwe wa Mbezi Beach wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kwa
zoezi hilo leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo ni harakati za kuunga
mkono kampeni ya kuiokoa Bahari ambalo limeshirikisha asasi za Nipe
Fagio, Mbezi Beach na Friends Of Ocean kutoka Mikocheni B chini ya
udhamini wa Nabaki Africa, Koncept Communication Pamoja na AFM 92.9 ya
mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment