MKUU wa Mkoa Wa Morogoro ,dk
.Kebwe Steven Kebwe ,akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa
Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,makabidhiano hayo yamefanyika eneo la
Bwawani mpakani mwa mikoa hiyo ,Mwenge wa Uhuru ukiwa Pwani ulitembelea
miradi 81 yenye thamani ya bil. 225.1
Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi
Evarist Ndikilo ,akikabidhiwa mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya
ya Bagamoyo ,alhaj Majid Mwanga ,kabla ya makabidhiano ya Mkoa huo na
Morogoro ,ambapo Mwenge ukiwa Bagamoyo ulitembelea miradi 22 ya bil.129
..(picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi ,Pwani
KIONGOZI wa mbio za
mwenge kitaifa ,Amor Hamad Amor ,ameupongeza mkoa wa Pwani kwa kusheheni
viwanda mbalimbali na kuiomba jamii ivitumie kwa lengo la kujikwamua
kiuchumi .
Aidha amewataka
wawekezaji kutoa ajira pale inapostahiki na kushiriki huduma za kijamii
kwenye maeneo yao husika ili wananchi waweze kunufaika nao .
Akizungumza wakati wa
makabidhiano ya mwenge wa uhuru kutoka Pwani kwenda mkoani Morogoro
,eneo la Bwawani ,Amor alisema wameagizwa kufanya kazi hivyo kwa mkoa wa
Pwani wameiona na wamefanyakazi .
Alieleza ,mkoa huo una
viwanda vya kutosha ambapo vinaendana na dhamira ya serikali ya awamu ya
tano ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda .
“Tumejionea baadhi ya
viwanda vinavyoendelea na ujenzi na vilivyokamilika ikiwemo cha vipodozi
,kile kinachotengeneza dawa za viuadudu vya malaria ,cha kusindika
matunda cha Sayona “
“Vya kuchakata mihogo
,vya kutengeneza vigae ambavyo vyote vitasaidia kwa kiasi kikubwa
kuinua mapato ya halmashauri, wilaya ,mkoa na taifa ” alibainisha Amor
.
Amor ,hakusita kuwataka vijana na makundi yote kufanyakazi na kuachana na tabia ya kukaa kimazoea .
Alisema ni wakati wa
kujiunga hata kimakundi kuanzisha viwanda vidogo na shughuli za
kijasiriamali ili kujikomboa na hali ya umaskini .
Nae mkuu wa mkoa wa
Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ,akimkabidhi mwenge huo ,mkuu wa mkoa wa
Morogoro dk.Kebwe Steven Kebwe ,alisema mkoa wake unatekeleza ukuaji wa
sekta ya viwanda na uwekezaji .
Mhandisi Ndikilo
,alieleza ,mkoa huo umejipanga kuwa ukanda wa viwanda kwani kitaifa kuna
viwanda vikubwa 304 huku kimkoa vikiwa 84 na vilivobakia ndio mikoa
mingine .
“Mkoa huu unatekeleza
kwa vitendo ujumbe wa mwenge “Shiriki kukuza uchumi wa Viwanda kwa
maendeleo ya nchi yetu” ambapo kwa sasa una viwanda 264”
“Kati ya hivyo viwanda
vikubwa ni 84 na vidogo 186 na kila Halmashauri imetenga maeneo kwa
ajaili ya uwekezaji na kuna mazingira mazuri kwa wawekezaji,” alisema
mhandisi Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo
,alipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Dar es salaam ,June mosi ambapo
umetembea halmashauri Tisa, miradi 81 yenye thamani ya sh.bil 225.1.
Kati ya miradi hiyo ,27 itawekewa mawe ya msingi, na miradi 27 itazinduliwa na minne itafunguliwa na miradi 25 itakaguliwa.
Alifafanua ,miradi hiyo yote imechangiwa kwa pamoja na wananchi, serikali kuu, Halmashauri na wahisani wa ndani na nje .
Awali mkuu wa mkoa wa
Pwani alikabidhiwa mwenge huo kutoka wilaya ya Bagamoyo, ambako Mkuu wa
wilaya hiyo ,alhaj Majid Mwanga ,alisema kumetembelewa miradi 22
iliyogharimu sh.Bilioni 129 ..
No comments:
Post a Comment