Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu
anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana amefungua mpango wa
mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa kwa
vijana 1000 wanaotaka mikoa zaidi ya kumi nchini.
Akizundua mpango huo, Mhe Mavunde, amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wa kujiajiri vijana na pia kutumia bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo kwa ajili ya kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi nchini.
Amesema, serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha inatekeleza azma ya ujenzi wa viwanda kwa kuwajengea uwezo vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa katika kujiandaa na mfumo wa mapinduzi ya viwanda ambavyo vimeshaanza kujengwa nchini.
Aidha amewataka vijana kutochagua kazi au kubweteka kuwa kazi rasmi ni zile za ajira ya moja kwa moja serikali au sekta binafsi, amewataka vijana kubadilisha mtazamo wa maaana ya Ajira kwa kutokukaa na kusubiri nafasi za ajira.

Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano.
Wizara ya kazi,ajira, ulemavu na maendeleo ya vijana
03/06/2017
No comments:
Post a Comment