Wazazi
wakiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na watoto wao waliozaliwa
kabla ya muda wakipatiwa huduma mbalimbali ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika.
Maadhimisho hayo yamefanyika kitengo cha watoto njiti katika hospitali hiyo.
Dar es salaam
Asilimia
98 ya watoto wanaozaliwa kabla ya siku na kutunzwa katika kitengo cha
watoto walipo kwenye matunzo ya Kangaroo Mother care katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) wanatoka salama na wakiwa na afya njema.
Hayo
yamesemwa LEO na Muuguzi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Rose
Mathew alipokuwa akizungumza na wazazi ambao wamefika Kiliniki na
kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika kwenye kitengo cha watoto ambao wapo
kwenye matunzo ya Kangaroo Mother care hospitalini hapo.
Amesema
matunzo ya Kangaroo Mother care yamesaidia kupunguza vifo vya watoto
wachanga wanaozaliwa kabla ya siku na kwamba kitengo hicho kilichopo MNH
kimekua faraja kwa wazazi.
“Hospitali
inapata faraja kwasababu matunzo ya Kangaroo Mother care yameonyesha
mafanikio makubwa katika hospitali yetu ikiwa ni njia mbadala ya matunzo
ya watoto wanaozaliwa kabla ya siku’’ amesema Muuguzi Rose Mathew.
Kwa
upande wao wazazi waliofika kilini hapo wametoa wito kwa uongozi wa
hospitali kuendelea kuboresha huduma hiyo kwasababu kituo hicho ni cha
taifa na kinahudumia watoto wengi.
Jumla ya watoto 47 waliokuwa kwenye matunzo ya Kangaroo Mother care leo wamehudhuria kilinikini wote wakiwa na afya njema .
No comments:
Post a Comment