
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward
Lowassa amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli alianza vizuri kwani
yapo mambo aliyoyafanya ni mazuri lakini pia yapo mambo mengine amefanya
yana matatizo.
Lowassa amesema haya alipokuwa akifanya mahojiano na kusema kwa sasa
tumuache Rais Magufuli aendelee na kazi yake lakini baadaye ndiyo watu
waweze kumuhukumu kutokana na mambo ambayo ameyafanya.
"Rais Magufuli ameanza vizuri kubana mambo mazuri amefanya lakini kuna
mambo mengine yana matatizo, lakini Mwalimu Nyerere aliwahi kusema
wakati unafagia, unaweza kufagia hata shilingi sasa Rais Magufuli
anafagia shilingi nyingi. Lakini tumuachie aendelee na kazi tumuhukumu
baada ya kipindi fulani" alisisitiza Lowassa
No comments:
Post a Comment