Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila
akizungumza na watumishi alipokua akiwaaga. Dkt. Kayandabila ameteuliwa
na Mhe. Rais kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania. (BoT).
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akipokea
zawadi, ikiwa ni ishara ya pongezi kwa uteuzi wake mpya alioupata.
Anayemkabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya watumishi wa wizara ni Naibu
Katibu Mkuu; Dkt Mosses Kusiluka.
Watumishi wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika picha ya pamoja na aliyekuwa Katibu
Mkuu wa wizara hiyo; Dkt. Yamungu Kayandabila mara baada ya kuwaaga.
Aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila
amesisitiza utumishi bora unaozingatia Miongozo na Sheria.
Dkt. Kayandabila aliyeteuliwa hivi
karibuni na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Naibu Gavana wa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), akiwaaga Watumishi wa Wizara alihimiza
utendaji bora kazini katika kutoa huduma kwa Wananchi na kusihi
Watumishi kuendelea na kasi hiyo.
Aidha, aliwashukuru Watumishi wa
Wizara ya Ardhi kwa ushirikiano wao walioonyesha kwake ambao
umesababisha kudhihirisha matukio chanya kwa Wizara. Alisema; “
Tukumbuke kuwa sisi ni Watumishi wa Umma, tuendelee kufanya kazi kwa
bidii kwa kuwahudumia Wananchi kwa bidii”.
Awali akizungumza kwa niaba ya
Watumishi wa Wizara; Afisa Mipango Miji, Baltazar Sumari alisema; “
Tunakushukuru Katibu Mkuu kwa jinsi ulivyotuwezesha kufanya kazi kwa
umoja na nidhamu, Mungu akuwezeshe uweze kuendelea kudumisha utendaji
wako wa kazi Benki Kuu kama jinsi ulivyofanya Wizarani hapa na
tutaendelea kuhitaji ushauri wako”.
Naye muwakilishi wa Taasisi za
Wizara; Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji (TPRB);
Helena Mtutwa alisema kuwa Dkt. Kayandabila ana karama ya kipekee ambayo
imemuwezesha kuongoza vyema kwa kuweza kuonyesha njia bora katika
utendaji kazi na kuonya kwa hekima.
Dkt. Kayandabila anakwenda kutumika katika Benki Kuu ya Tanzania kama Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha (Economic and Financial Policies – EFP),
akiwa na Naibu Gavana mwenza aliyeteuliwa naye kwa kipindi kimoja; Dkt.
Bernard Yohana Kibese atakayehusika katika eneo la Uthabiti na
Usimamizi wa Sekta ya Fedha (Financil Stability and Deepening – FSD).
Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaz
No comments:
Post a Comment