Tuesday 30 May 2017

Kufuatia Ghasia zinazoendelea Sudan kusini, Wanawake wakimbia makazi


wanawake na Watoto wazidi kuikimbia Sudan kusini
Maelfu ya wanawake na watoto kutoka Sudan kusini wamevuka mpaka kuingia nchini Sudan tangu kuanza kwa mwaka huu, wakikimbia ghasia na kitisho cha njaa.
Kwa mujibu wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi Duniani -UNHCR- Karibu Wasudan kusini laki moja na 37 elfu wameingia nchini Sudan tangu Januari mosi, huku wengine zaidi ya laki moja na 31 elfu wakiwa tayari wamewasili nchini humo tangu mwaka 2016.
Wafanyakazi wa misaada wanaarifu kuwa wengi ya watu hao wanaowasili sasa ni wanawake na watoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Msalaba mwekundu, kanda ya Afrika Dokta Faroumata Nafo-Traore wengi wanakuwa wamedhoofika kiafya na wamekuwa na msongo wa mawazo kutokana na hali iliyowatokea huko wanakotoka.

Tangu Desemba mwaka 2013 jumla ya wakimbizi laki nne na 17 elfu wa Sudan Kusini waliingia nchini Sudan. Wengi wao wako katika kambi zilizokuwa Mashariki na Kusini mwa Darfur na magharibi na kusini mwa Kordofan.

No comments:

Post a Comment